Mabingwa wa Ligi Kuu bara Yanga SC usiku huu wametwaa kombe la CRDB Cup 2024/2025 baada ya kuichapa Singida Black Stars mabao 2-0 katika mchezo wa fainali uliofanyika uwanja wa New Amaan Stadium Zanzibar.
Dakika ya 39 kiungo mkabaji Duke Abuye raia wa Kenya alitangulia kwa kuipatia bao Yanga kabla ya Clement Francis Walid Mzize kuandika bao la pili dakika ya 49.
Hata hivyo mshambuliaji wa Singida Black Stars Jonathan Sowah raia wa Ghana alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 86 na mwamuzi Ahmed Arajiga.
Huu ni ubingwa wa nne mfululizo kwa Yanga kwenye kombe hilo historia ambayo wameiandika kwa mara ya kwanza tangu kuanzishwa michuano hiyo na pia kwa hapa nchini kuwa timu ya kwanza kutwaa mara nne mfululizo.
Ikiwa katika msimu huu imetwaa makombe matano ambayo ni pamoja na kombe la TUYOTA, Muungano, Ngao ya Jamii na Ligi Kuu bara.