KLABU ya Azam FC imetangaza kuachana na winga wake Mgambia, Gibril Sillah (26) baada ya misimu miwili ya kuwa na timu hiyo kwa misimu miwili na nusu.
Kupitia kurasa zake za mitandao ya kijamii, Azam FC imemuaga na kumshukuru Sillah ambaye naye pia kwenye kurasa zake amefanya hivyo.
Kwa mujibu wa Azam FC, katika kipindi cha misimu miwili na nusu, Sillah amecheza jumla ya mechi 68 akifunga mabao 21 na kutoa pasi za mabao 10 yaliyofungwa na wengine.
Sillah ameandika kuishukuru Azam FC akisema; “Asanteni Azam Football Club kwa yote mliyonifanyia katika kipindi hiki cha miaka miwili,”.