Klabu ya Mbeya City ya jijini mbeya ipo katika mazungumzo na Winga wa Klabu ya Yanga SC, Faridi Musa , ambae tayari mkataba wake upo ukingoni kumalizika katika Klabu ya Yanga SC.
Faridi Musa amekuwa na nafasi finyu katika Kikosi cha Yanga msimu uliomalizika jambo ambalo limemfanya kupoteza nafasi kabisa katika Kikosi cha Yanga SC.
Mbaya City ambayo imepanda ligi msimu huu tayari wameanza kufanya usajili kwenye Kikosi chao ili kuifanya Klabu hiyo Kuwa na msimu mzuri ujao kwenye ligi kuu Tanzania bara.