Simba Sports Club imeachana rasmi na kiungo wao raia wa Congo Brazzaville, Debora Mavambo, baada ya muda mfupi wa kuitumikia klabu hiyo.
Hatua hii ni sehemu ya mabadiliko makubwa yanayotarajiwa ndani ya kikosi cha Simba kwenye dirisha hili la usajili, ambapo taarifa zinaeleza kuwa wachezaji wengine watakaoachwa watajulishwa hibi karibuni.
Mavambo alijiunga kama kiungo mwenye matumaini, lakini safari yake imefikia ukomo kabla ya msimu mpya wa 2025/26.