“Nianze na pole kwa Wana Simba kumaliza msimu bila ubingwa katika mashindano tuliyoshiriki hususan ligi kuu ya NBC. Wana Simba tuepuke presha za wanaotuaminisha tumefeli kupita kiasi
Ni kweli hatujapata ubingwa lakini sote ni mashahidi kuwa timu yetu imepiga hatua kubwa sana kulinganisha na miaka ya nyuma na hilo ndio lilikua lengo letu kutengeneza timu ya ushindani. Msimu huu tumefanikiwa kucheza Fainali ya CAF ambayo tumeshindwa kufanya hivyo kwa miaka 31
Msimu huu ubingwa wa ligi umeamuliwa na Dkk 45 za Kipindi cha pili cha mechi ya mwisho, wakati msimu uliopita tulipigania nafasi ya tatu. Points tulizofikisha msimu huu hatujawahi kufikisha kwa miaka minne iliyopita.
Tulipotoka na tulipo ni tofauti sana, mwangaza wa mafanikio hauko mbali yetu. Si mara ya kwanza Simba kukaa miaka minne bila Ubingwa, tushakaa miaka mitano kutoka 2012 hadi 2017 lakini tulijipanga 2018 tukachukua kwa miaka Minne mfululizo.
Kupoteza mara 5 mfululizo dhidi ya Mtani kusitufanye tukajidharau. Madrid amepoteza El Classico nne dhidi Barcelona tena kwa vipigo vya vikali lakini katu huwezi kuwaona wanajitukana.
Sio mfano wa kujivunia lakini lazima tukubali nyakati hizi hutokea kwenye mpira. Pamoja na ukubwa wote Manchester United wanaenda mwaka wa 13 bila Ubingwa, Sitaki kutoa mfano wa Arsenal
Mifano hii itupe taswira kuwa hatuko peke yetu kwenye mapito ya namna hii na hata hawa wanaocheka sasa yapo magumu waliyopitia
Ombi langu wangu Wana Simba, tuwape nafasi viongozi wetu wafanye tathmini na baada ya hapo watupe muongozo tunaendaje mbele kuipambania Simba yetu.
Heshima yetu itarudi kwa kushikamana na kusimama pamoja