Licha ya kufanya vizuri kwenye michezo miwili dhidi ya Simba na Singida Black Stars, Duke Abuye anatarajia kuondoka Jangwani na msimu ujao ataonekana nchini Algeria.
Kiungo huyo aliyecheza vizuri zaidi kwenye mchezo wa dabi ya Kariakoo akiziba vema nafasi ya Khalid Aucho huku Yanga ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 na jana akicheza vizuri dhidi ya Singida huku Yanga ikishinda tena mabao 2-0 na yeye akifunga bao la kwanza dakika ya 39.
Mkataba wake wa mkopo alitokea Polisi ya Kenya ingawa Yanga alitua akitokea Singida Black Stars, tayari klabu ya JS Kaybilie ya Algeria imeshamalizana na Polisi na kinachosubiriwa na kumalizika kwa shughuri za kufunga msimu na Yanga ikiwa imeshinda Mataji matano msimu huu.