Rais wa klabu ya Yanga SC, Injinia Hersi Said na Makamu wake Arafat Haji wote wawili wamejitosa kwenye ulingo wa siasa na watagombea ubunge.
Tayari Injinia Hersi amechukua fomu ya kugombea ubunge katika Jimbo la Kigamboni jijini Dar es Salaam kupitia Chama Cha Mapinduzi, CCM wakati Arafat anatarajia kuchukua fomu kwenye Jimbo la Shaurimoyo, Zanzibar.
Hii yote inatokana na Rais Samia Suluhu Hassan kuwa mwanamichezo hivyo wanamichezo wengi wameamua kujitosa kwenye majimbo kuwania ubunge.