TIMU ya Paris Saint-Germain ya Ufaransa imefanikiwa kuingia Robo Fainali ya Kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya wenyeji, Inter Miami CF usiku huu Uwanja wa Mercedes-Benz, Atlanta, Georgia.
Mabao ya mabingwa hao wa Ulaya, PSG yamefungwa na kiungo Mreno, João Neves mawili, dakika ya sita na 39, Mabeki, Muargentina Tomás ‘Toto’ Avilés aliyejifunga dakika ya 44 na Mmorocco, Achraf Hakimi dakika ya 45+3.