Supastaa wa Barcelona mwenye umri wa miaka 17, Lamine Yamal hivi majuzi ameshangaza watu wakati wa mapumziko yake ya msimu huu wa joto kwenye Kisiwa cha Ibiza (Hispania).
Yamal alinaswa akiwa likizoni kwenye boti ya kifahari huko Ibiza kwa gharama ya kukodisha inayokadiriwa kuwa euro 5,000 sawa na milioni 15 za kitanzania kwa siku, ambapo Kwenye boti hiyo, alienda marafiki zake pamoja na wasichana wachanga wapatao 8 ambao aliwaalika kufurahia nao.
Picha kutoka kwenye boti hiyo zinaonesha Yamal akiwa hana shati, akipiga picha na wasichana hao waliovalia bikini, zimesababisha taharuki mtandaoni. Watu wengi wakionesha kushangazwa na kutilia shaka maisha ya anasa ya mwanasoka huyo mchanga.
Bila shaka, Yamal yuko kwenye likizo ya majira ya joto na anaweza kufurahia atakavyo kabla ya kurudi uwanjani msimu ujao. Lakini mashabiki wengi hawawezi kujizuia kuwa na wasiwasi kuhusu mustakabali wa staa huyu wa soka, hasa wanapomlinganisha na kizazi cha mfano cha Messi, Iniesta.