Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2026

Makonda amteua Leodgal Tenga kamati ya AFCON

Picha
WAZIRI wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Christian Makonda amemteua Nahodha wa zamani wa timu ya soka ya taifa ya Tanzania, Leodegar Chilla Tenga kuwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ndani ya Maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2027 ambazo Tanzania inaandaa kwa ushirikianona majirani, Kenya na Uganda.

Simba yaendeleza vipigo Sheikh Amri Abeid

Picha
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo Mzambia, Clatous Chotta Chama dakika ya 45’+7, winga Msenegal Libasse Gueye dakika ya 53 na kiungo mzawa, Shaaban Mgunda aliyejifunga dakika ya 71 wakati akijaribu kuokoa. Kwa matokeo hayo, Simba SC inafikisha pointi 39, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi tano na mabingwa watetezi, Yanga SC baada ya timu zote kucheza mechi 18. Kwa upande wao Fountain Gate baada ya kupoteza mchezo wa 10 leo kati ya michezo 18 iliyocheza hadi sasa, mingine minne ikitoaa sare na kushinda minne pia – inabaki na pointi zake 16 nafasi ya 14 katika ligi ya timu 16. Ikumbukwe mwisho wa msimu timu mbili zitashuka Daraja na mbili zitakazomaliza nafasi ya 14 na 13 zitamenyana baina yao kwa mechi mbili za nyumbani na ugenini na mshindi wa jumla atasalia Ligi Kuu. Timu itakayofungwa itakwenda...

Uwanja wa Yanga wafikia pazuri

Picha
Rais wa klabu ya Yanga SC, Eng Hersi Said ameweka bayana suala la ujenzi wa uwanja wa Yanga SC utakaojengwa Jangwani, umefikia pazuri. "Kwenye ujenzi wa uwanja tumefika kwenye eneo zuri sana. Tunafanya mchakato wetu kwa umakini mkubwa na kwa usahihi. "Tuliwatangaza GSM kuwa washindi wa tenda ya ujenzi wa uwanja. Tayari tumepata mchoro wa awali wa uwanja.  Klabu imeshatoa maoni kuhusu mchoro huo. Jana tumekamilisha michoro yote na gharama za ujenzi” Eng Hersi Said @caamil_88, Rais wa Klabu ya Yanga SC

Muhibu Kanu kuendelea kuwa kocha mkuu Singida Black Stars

Picha
Uongozi wa Klabu ya Singida Black Stars umefikia makubaliano ya kumuajiri aliyekuwa Kocha wa AS Maniema, Papy Kimoto kuwa Meneja Mkuu wa Timu, pamoja na Kapiten Ngoyi Dora kuwa Kocha Msaidizi, wote wakisaini mikataba ya mwaka mmoja na miezi mitatu. Aidha, Muhibu Kanu ataendelea kushika nafasi ya Kocha Mkuu hadi mwisho wa msimu huu, akisimamia kikamilifu majukumu ya kiufundi kwa kushirikiana na safu mpya ya Benchi la Ufundi.

UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI - 13

Picha
Inaandikwa na Fikiri Salum Ilipoishia  KUHUSU maeneo ambako Wakristo wanapungua ni kwamba kutokana na historia ya kanisa kuwa na mchanganyiko wa mazuri na mabaya, wengine wanahisi kuwa halina maana tena. Endelea Pia Kuna makundi kama Wakomunisti na Wamasoni ambayo yanakusudia kabisa kufuta Ukristo kwa kutangaza kasoro za waumini na viongozi wao, pamoja na kuhimiza watu kwenda kinyume cha maadili. Hali hii inajionyesha hasa pale ambapo waamini wengi, hasa Ulaya, wameacha kwenda kanisani isipokuwa siku ya Krismasi na Pasaka au kwenye harusi na msiba. Pia kutokana na mgawanyiko wa madhehebu kumekuwa na mkanganyiko kuhusu kazi ambazo zinaipasa kanisa la leo. SALA NA IBADA Mafundisho ya Yesu kuhusu sala hayatii maanani taratibu maalum, badala yake yeye alisisitiza msimamo wa ndani wa kumuendea Mungu kwa imani na unyofu kama vitoto vinavyohusiana na baba zao. Ndivyo mwenyewe alivyosali katika roho mtakatifu aliyewaahidia wafuasi atawaongoza badala yake. Kwa msingi huo, katika historia ya kan...

Dkt Mwinyi atembelea mradi wa AFCON mkoa Mjini Magharibi

Picha
Rais wa Zanzibar, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, ameutembelea mradi wa Mji wa AFCON Fumba uliopo Mkoa wa Mjini Magharibi. Ziara hiyo imefanyika leo Aprili 14, 2026, akiambatana na Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo, Dkt. Riziki Pembe Juma, pamoja na wadau wa mradi wa AFCON Fumba Zanzibar. Katika ziara hiyo, Rais Dkt. Mwinyi amekagua maeneo mbalimbali ya uwanja huo wa kisasa wa AFCON unaojengwa na kampuni ya ORKUN GROUP ya Uturuki, ambao unaotarajiwa kutumika kwa michuano ya #AFCON2027 itakayofanyika kwa ushirikiano wa nchi tatu za Afrika Mashariki za Kenya, Uganda na Tanzania. Aidha Dkt. Mwinyi ametembelea na kukagua miundombinu inayotarajiwa kujengwa kuzunguka uwanja huo, ikiwemo hospitali, barabara, migahawa, maduka makubwa (mall) pamoja na huduma nyingine muhimu zitakazouzunguka mji huo wa kisasa. Uwanja huo unakadiriwa kuchukua watazamaji elfu 35, ukiwa na viwango vya ubora vinavyokubalika na Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF).

Magori aungana na Simba kula nyama choma Arusha

Picha
Mwenyekiti wa Bodi, Crescentius Magori na Mjumbe wa Bodi, Dr. Seif Muba wamefika hapa katika Simba Nyama Choma Festival hapa Arusha.

Simba yamrejesha kikosini Jonathan Sowah

Picha
Simba SC wamemrejesha rasmi mchezaji wao Sowah kwenye kikosi cha klabu hiyo baada ya kipindi cha kutokuwa sehemu ya timu ya kwanza. Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana, uongozi wa Simba umeamua kumpa nafasi nyingine mchezaji huyo huku ukimwelekeza kuanza mazoezi na kikosi cha vijana chini ya umri wa miaka 20 (U-20). Hatua hiyo inaonekana kuwa sehemu ya mpango wa kumjengea upya utimamu wa mwili, nidhamu na kurejesha kiwango chake kabla ya kujiunga tena na kikosi cha wakubwa. Sowah anatarajiwa kuonyesha uwezo wake katika mazoezi hayo ili kushawishi benchi la ufundi kumpa nafasi ya kurejea kwenye timu ya kwanza katika mechi zijazo.

Klabu ya Ligi Kuu Burkina Faso yaja kujifunza Young Africans

Picha
Timu ya soka ya Usfaburkina kutoka Ouagadougou inayishiriki Ligi Kuu nchini Burkina Faso imewasili makao makuu ya klabu ya Yanga SC kwaajili ya Semina ya Mafunzo ya mfumo wa uendeshaji wa klabu ya mpira wa miguu. Mafunzo hayo yameanza leo chini ya idara ya Wanachama na Masoko kisha kuendekea kesho kupitia idara nyingine kabla ya kuhitimisha semina hii na kukutana na Rais wa Yanga Eng Hersi Said.

UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI - 12

Picha
Inaandikwa na Fikiri Salum Ilipoishia  KWA kweli karne za kati zilikuwa na mchanganyiko wa mambo yaliyopingana ibada za nje tu na za shati kabisa teolojia iliyoelekeza kutenda kwa msingi wa nipe nikupe na hakika ya kwamba binadamu anategemea kabisa neema ya Mungu. Endelea Kutojali wajibu hata upande wa viongozi wa kanisa na marekebisho safi ya mashirika ya kitawa. Karne ya 15 ilikuwa kipindi cha umo motomoto wa pekee katika kanisa, ambapo walei wengi zaidi na zaidi walipata aimu nzuri, hivyo walitamani hotuba bora na mafundisho ya kuwasaidia kuishi Kikristo zaidi. Luther aliitikia haja hizo zilizomgusa sana kama mtu wa wakati wake Luther alitumia kwa nadra neno urekebisho, lakini ukaja kuwa jina la kawaida la matukio yale mengi ya miaka 1517- 1555. Yaani kuanzia uenezi wa hoja 95 za Martin Luther hadi amani ya Augsburg , kati yake chanzo, yaani mabishano ya kikamisa yaliyosababishwa na teolojia ya Luther, yalichanganyika mapema na sasa. Uchumi na utamaduni, kutokana na hali halisi ya w...

Fikiri Elias awa kocha mkuu Coastal Union

Picha
Fikiri Elias Mahiza amejiunga na klabu ya Coastal Union akiwa ndiye kocha mkuu wa klabu hiyo akichukua mikoba ya Mohamed Muya. Hii sio mara ya Kwanza Kwa Fikiri kuwa kocha mkuu kwenye kikosi hicho kwani mwaka 2023 alikuwa ndiye kocha mkuu huku pia akiwahi kuwa kocha msaidizi wa klabu hiyo chini ya kocha Mwinyi Zahera. Fikiri Elias amewahi kufundisha timu za JKT Oljoro na Kengold ikumbukwe kuwa Kwa sasa Fikiri ni miongoni mwa makocha waliopo kwenye idara ya Ufundi ya TFF lakini ni Mkufunzi wa makocha Kwa ngazi ya CAF na FIFA

Kocha JKT Queens amlilia straika wake

Picha
Kocha wa JKT Queens, Kessy Abdallah amesema kukosekana kwa mshambuliaji wake tegemeo, Winifrida Gerald kumewaathiri kwa kiasi kikubwa kutokana na umuhimu wake katika safu ya ushambuliaji. Winifrida anayeongoza kwa ufungaji wa mabao ndani ya JKT Queens akiwa na Mabao 8, alifungiwa mechi tatu na faini ya Sh500,000 kwa kumshambulia beki wa Geita Queens. "Ni mchezaji muhimu tena sana, kimetuathiri kwa sababu hata wenzake wanamtegemea, kwa hiyo ilikuwa kazi kubwa sana kuwaelewesha kuwa tunaweza kufanya kitu bila yeye,” alisema Kessy. Aliongeza changamoto kubwa haikuwa tu kiufundi bali pia kisaikolojia kwa wachezaji wengine, ambao walipaswa kujijenga upya kujiamini na kucheza kwa mshikamano zaidi. "Baadae walinielewa na kweli tumeweza kufanya vizuri michezo miwili bila yeye na nashukuru Mungu na tunaamini tutafanya vizuri,” aliongeza. Pamoja na mafanikio hayo, Kessy alikiri ushindani katika mechi zao umekuwa mkubwa, huku kila timu ikipambana kwa nguvu kutafuta ushindi. “Vijana wana...

Abdi Banda akumbushia alivyoondoka Simba kwa mbinde

Picha
Beki Kisiki Abdi Banda anasema watu wasichojua wakati anasajiliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini, alisubiri barua ya Simba kumruhusu kuondoka tangu alfajiri mpaka jioni katika ofisi za klabu hiyo wakati huo zipo Posta lakini hakuipata n kesho yake ana ticket ya ndege ili kurejea nchini humo. "Sikula kutwa nzima, baadhi ya viongozi walikuwa wakinipita tu kwenye wakati ilikuwa ni jambo dogo sana juu ya barua yangu, ilinikasirisha maana sikuwa nimefanya jambo baya, nilifuata utaratibu ila hakuna aliyenipa msaada mpaka kiongozi Mmoja wa Simba aliyepiga simu kutoka nje ya nchi na kuahidi atafatilia hivyo naweza nikaondoka" "Nilipofika airport, Waandishi walinihoji, sikuficha nilielezea ukweli wote sasa kusema kuwa viongozi wameninyima barua ndiyo ikawa kosa kuambiwa nimeitukana Simba" "Embu niambie hapo kosa langu ni nini? Kusema ukweli?" Ameniambia Banda.

Masikini, Camara aonyeshewa mlango wa kutokea Simba

Picha
Klabu ya Simba imefikia makubaliano ya kuachana na mlinda mlango wake, Moussa PinPin Camara (27), kuelekea msimu mpya wa ligi wa 2026/27. Uamuzi huo umekuja huku uongozi wa klabu hiyo ukiamua kuendelea kumpa imani mlinda mlango namba moja kwa sasa, Gibrilar Kassali, ambaye amekuwa na kiwango bora langoni. Camara, ambaye aliondolewa kwenye mfumo wa wachezaji wa klabu hiyo wakati wa dirisha dogo la usajili kufuatia majeraha makali aliyoyapata kwenye michuano ya kimataifa mwanzoni mwa mwaka huu, tayari amearifiwa kuwa hatatunukiwa mkataba mpya na hivyo yuko huru kutafuta changamoto nyingine. ​Kuondoka kwa mlinda mlango huyo kunahitimisha safari yake ya miaka miwili pekee ndani ya klabu ya Simba tangu alipojiunga nayo. Ikumbukwe kuwa licha ya changamoto za majeraha zilizomuweka nje ya uwanja kwa muda mrefu, klabu ya Simba ilisimamia na kugharamia matibabu yake yote hadi kuhakikisha amepona kikamilifu na kurejea katika hali yake ya kawaida.

Kyombo aanza na ushindi kiduchu Zambia

Picha
Nyota wa Tanzania Habib Kyombo akiwa na timu yake ya NAPSA FC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya FC Leopards kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Zambia. Kyombo licha kwamba amewahi kuichezea Simba SC ya Tanzania na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini, lakini aliibuka akitokea timu ya Mbao FC ya mkoani Mwanza nchini Tanzania.

UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI - 11

Picha
Inaandikwa na Fikiri Salum Ilipoishia  HIYO ilitokana na msimamo wa msingi wa urekebisho wa Kiprotestanti wa kutaka kila mmoja aweze kutafsiri Biblia alivyoielewa bila kutegemea mapokeo wala mamlaka rasmi ya kanisa, ila msaada wa roho mtakatifu  Endelea Umoja halisi wa kanisa unaweza kupatikana tu katika ukweli wa injili ya Yesu Kristo, ni habari mbaya kwamba katika karne ya 16 kuupigania ukweli huo kulivunja umoja wa Ukristo wa magharibi, haiwezekani kushangilia mafarakano ya wafuasi wa Yesu. Yake ya karne hiyo yalitokana na kuelewa tofauti kweli za imani ya Kikristo na yalikuwa na ukali kwa sababu pande zote zilisadiki kwamba kushikilia kwa usahihi ufunuo wa Mungu ni suala la wokovu wa milele. Kwa mfano Martin Luther aliandika sikubali mafundisho yangu yahukumiwe na yeyote, hata kama ni malaika, asiyekubali mafundisho yangu hawezi kufikia wokovu (11). Pamoja na hayo, mambo mengi yalichangia farakano, si Teolojia tu bali siasa, uchumi, jamii na utamaduni, wakati huo mara nyingi hoja z...

Samatta afunga bao lake la kwanza Ufaransa

Picha
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania Mbwana Sammata leo amefunga goli lake La kwanza tangu ajiunge na Le havre ya nchini ufaransa dhidi ya OG Nice Samatta ameweka rekodi ya kuwa Mtanzania wa kwanza kufunga Goli ligi kuu nchini Ufaransa.

Azam FC yaichakaza Fountain Gate 4-0

Picha
Klabu ya Azam imetinga robo fainali ya Kombe la Shirikisho la CRDB (FA Cup) kufuatia ushindi wa 4-0 dhidi ya Fountain Gate FC katika dimba la Azam Complex, Chamazi kwenye mchezo wa hatua ya 16 bora. Wanalambalamba hao wameungana na Simba, Yanga, Coastal Union, JKT Tanzania, TRA United, Singida BS na Mashujaa kwenye hatua hiyo. Mabao ya Azam FC yamefungwa na Japhte Kitambala dakika ya 15, Abah Abbel dakika ya 21, Ashrafu Kibeku dakika ya 81 na Alobigast Kyobya dakika ya 90.

Simba yakata ngebe za Dodoma Jiji

Picha
TIMU ya Simba SC imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC jioni ya leo Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arisha. Mabao ya Simba SC yamefungwa na mshambuliaji Suleiman Abdallah Mwalimu mawili dakika ya 54 na 67 na winga wa kushoto Muivory Coast, Alain Anicet Oura dakika ya 60 baada ya kiungo Khleffin Salum Hamdoun kuanza kuifungia Dodoma Jiji FC dakika ya tisa.

Aziz Ki azidi kuwasha moto Libya

Picha
Stephanie Azizi Ki leo ameendelea kuonesha makali yake kwenye ligi kuu ya Libya akiwa na klabu yake ya Al-Ittihad SC. Aziz Ki leo amefanikiwa kufunga bao 1 kwenye ushindi wa mabao 4-1 walioupata Al-Ittihad dhidi ya klabu ya Shabab Al Ghal kwenye mchezo wa ligi kuu ya Libya. Hili sasa linakuwa ni goli lake la pili kwenye michezo 6 aliyocheza mpaka sasa ndani ya klabu hiyo kwenye ligi kuu msimu huu.

Singida Black Stars siyo ya mchezo mchezo, yaiua Mbeya City 5-1

Picha
TIMU ya Singida Black Stars imefanikiwa kwenda Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 5-1 dhidi ya Mbeya City Uwanja wa Airtel Mwigulu mjini Singida. Mabao ya Singida Black Stars yamefungwa na Khalid Aucho, winga wa kulia Mgambia, Lamin Jarjou, beki wa kushoto Mghana Ibrahim Imoro mawili na mshambuliajii kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Malanga Horso Mwaku.

TRA yaiua Namungo pale pale kwa Majaliwa

Picha
TIMU ya TRA United imetinga Robo Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC jioni ya leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao yote ya TRA United inayofundishwa na Kocha wa zamani wa timu ya taifa ya Tanzania, Mrundi Etienne Ndayiragijje yamefungwa na wachezaji wazawa, winga Denis Nkane na kiungo Ally Ng'azi.

Maximo: KMC itashuka daraja

Picha
Kocha Mbrazili Marcio Maximo ameibuka na kutoa ukweli mchungu kuhusu hali ya KMC FC inayozidi kuporomoka kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara. Baada ya kuondoka kwa Abdallah Mohamed ‘Bares’ (aliyechukua nafasi ya Maximo), Maximo ameweka wazi kuwa tatizo la KMC ni kubwa kuliko mwalimu yeyote: Makosa ya Msingi: Maximo amekiri kuwa yalifanyika makosa wakati wa maandalizi ya mwanzo wa msimu (Pre-season) kipindi yeye akiwa kocha mkuu. Ubora wa Wachezaji: Amesema baadhi ya wachezaji kikosini hawana ubora wa kuhimili presha ya ushindani wa Ligi Kuu. Hali ya Hatari: KMC sasa inashika mkia (nafasi ya mwisho) ikiwa na pointi 8 pekee baada ya mechi 18, huku ikiruhusu mabao 33! "Ingekuwa inawezekana, msimu ungeanza upya ili kikosi kiandaliwe upya, lakini kwa sasa timu itaendelea kubeba matatizo yaleyale," amesema Maximo kupitia gazeti la Mwanaspoti

Wachezaji saba wa Eritrea watokomea Eswatini

Picha
Wachezaji saba kutoka kikosi cha soka cha Eritrea kilichopata ushindi wa kihistoria nchini Eswatini wiki iliyopita hawajarejea nyumbani. Wakati baadhi ya wachezaji wenzao walirejea kutoka Afrika Kusini, jirani wa Eswatini, inadaiwa kuwa wachezaji hao saba wametoweka. Kumekuwa na matukio kadhaa katika miaka ya hivi karibuni ambapo raia wa Eritrea wanaoshiriki michezo mbalimbali hawajarejea nyumbani baada ya mashindano ya kimataifa. Makundi ya haki za binadamu yameelezea serikali ya Asmara kuwa ni yenye ukandamizaji mkubwa — tuhuma ambazo mamlaka zimekuwa zikizikanusha. Licha ya kuwa na idadi ndogo ya watu, mamia ya maelfu ya Waeritrea wamekimbilia kuomba hifadhi nje ya nchi. Habari za kutoweka kwa wachezaji hao ni pigo kwa timu hiyo, ambayo baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Eswatini na ushindi wa jumla wa 4-1, ilikuwa ikisherehekea kurejea katika hatua ya makundi ya kufuzu Kombe la Mataifa ya Afrika kwa mara ya kwanza baada ya miaka 19. Kati ya kikosi cha wachezaji 24, ni wachezaji 10 pe...

Loemba kuwaburuza Simba, FIFA

Picha
Klabu ya Colombe Sport wamekiri kuwa hawajalipwa pesa za usajili wa mchezaji Inno Jospin Loemba anayechezea klabu ya Simba SC ya Tanzania. Ikumbukwe huyu Inno Loemba ndiye mchezaji aliyesajiliwa na Mzabuni wa jezi wa klabu ya Simba Joe Rwegasira . Kwa mujibu wa Emmanuel Mwayombo, Makubaliano ya malipo yalikuwa klabu ya Simba itamalizia malipo ya usajili wa mchezaji tarehe 30 Machi. Mpaka sasa ni April 10 klabu ya Colombe haijapata kiasi hicho cha pesa…

Kocha wa zamani KenGold kumrithi Muya, Coastal Union

Picha
Kocha wa zamani wa Ken Gold,Fikiri Elias yupo mbioni kujiunga na Coastal Union ili kuchukua nafasi ya Mohamed Muya aliyeondoka klabuni hapo siku za hivi karibuni Fikiri Elias sio mgeni viunga vya Tanga na maeneo yake,aliwahi kuifundisha Coastal miaka ya 2023 hivyo anerejea tena kwa mara ya pili ili kuwapa ubora zaidi kwenye Ligi Kuu bara.

Simba kumwania mshambuliaji wa Stade Malien

Picha
Klabu ya Simba inamtazama mshambuliaji wa Stade Malien Taddeus Fomakwang Nkeng (26) kama chaguo la kuimarisha safu ya ushambuliaji kuelekea msimu ujao. Nyota huyo aliefanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika akifunga mabao 3 ameisaidia klabu yake kufuzu hatua ya Robo fainali kwa mara ya kwanza.

UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI - 10

Picha
Inaandikwa na Fikiri Salum ISIPOKUWA kwa kuwaachia watawale Italia ya kati, walisababisha Papa aanze kuwa kama Mfalme wa dunia hii, jambo lililoathiri sana majukumu yake ya kiroho hadi mwaka 1870. Endelea Katika karne za kati Ulaya yote ilikwisha kuwa ya Kikristo, kutoka huko ilienea, pamoja na ustaarabu wa magharibi, ulioathiriwa sana na Ukristo katika Amerika yote na sehemu nyingine za dunia. MAFARAKANO MAKUU KATI YA WAKRISTO Katika historia ndefu ya Ukristo, yalitokea mafarakano mengi waamini wa Yesu wakizidi kutofautisha, makundi makubwa zaidi ni kanisa katoliki, Makanisa ya Waorthodoksi na ya Waorthodoksi wa mashariki na madhehebu ya Uprotestanti, hasa tangu mwaka 1910 madhehebu mengi yanashiriki juhudi za Ekumeni kwa ajili ya kurudisha umoja wa awali. WAKATOLIKI Zaidi ya nusu ya Wakristo wote wanashikamana katika imani na sakramenti chini ya Maaskofu wenye ushirika kamili na yule wa Roma, ambaye kwa kawaida anaitwa Papa. Kati yao umoja unazingatiwa sana kama sifa ya kwanza ya kan...

Timu ya akina Kibu Denis yachapwa huko Libya

Picha
Baada ya michezo 12 kupita bila ya kupoteza mchezo wowote ule kwa timu ya Al-Nasry ndani ya group 4 la ligi kuu ya Libya msimu huu, hatimae leo wamepoteza mchezo. Al-Nasry leo wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu kwa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Al-Wafaq. Licha ya kipigo hicho Al-Nasry bado inandelea kusalia kileleni mwa group 4 wakiwa na alama zao 31 walizozipata kwenye michezo 12 waliyocheza mpaka sasa. Nyota wa zamani wa Simba SC, Kibu Dennis, Steven Mukwala na Fabrice Ngoma wote kwa pamoja walikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo huo. Na hiki sasa ndicho kipigo cha kwanza cha Al-Nasry toka Kibu na Mukwala wajiunge rasmi na klabu hiyo.