Loemba kuwaburuza Simba, FIFA
Klabu ya Colombe Sport wamekiri kuwa hawajalipwa pesa za usajili wa mchezaji Inno Jospin Loemba anayechezea klabu ya Simba SC ya Tanzania.
Ikumbukwe huyu Inno Loemba ndiye mchezaji aliyesajiliwa na Mzabuni wa jezi wa klabu ya Simba Joe Rwegasira .
Kwa mujibu wa Emmanuel Mwayombo, Makubaliano ya malipo yalikuwa klabu ya Simba itamalizia malipo ya usajili wa mchezaji tarehe 30 Machi.
Mpaka sasa ni April 10 klabu ya Colombe haijapata kiasi hicho cha pesa…
