Maximo: KMC itashuka daraja
Kocha Mbrazili Marcio Maximo ameibuka na kutoa ukweli mchungu kuhusu hali ya KMC FC inayozidi kuporomoka kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara.
Baada ya kuondoka kwa Abdallah Mohamed ‘Bares’ (aliyechukua nafasi ya Maximo), Maximo ameweka wazi kuwa tatizo la KMC ni kubwa kuliko mwalimu yeyote:
Makosa ya Msingi: Maximo amekiri kuwa yalifanyika makosa wakati wa maandalizi ya mwanzo wa msimu (Pre-season) kipindi yeye akiwa kocha mkuu.
Ubora wa Wachezaji: Amesema baadhi ya wachezaji kikosini hawana ubora wa kuhimili presha ya ushindani wa Ligi Kuu.
Hali ya Hatari: KMC sasa inashika mkia (nafasi ya mwisho) ikiwa na pointi 8 pekee baada ya mechi 18, huku ikiruhusu mabao 33! "Ingekuwa inawezekana, msimu ungeanza upya ili kikosi kiandaliwe upya, lakini kwa sasa timu itaendelea kubeba matatizo yaleyale," amesema Maximo kupitia gazeti la Mwanaspoti
