Kocha wa zamani KenGold kumrithi Muya, Coastal Union
Kocha wa zamani wa Ken Gold,Fikiri Elias yupo mbioni kujiunga na Coastal Union ili kuchukua nafasi ya Mohamed Muya aliyeondoka klabuni hapo siku za hivi karibuni
Fikiri Elias sio mgeni viunga vya Tanga na maeneo yake,aliwahi kuifundisha Coastal miaka ya 2023 hivyo anerejea tena kwa mara ya pili ili kuwapa ubora zaidi kwenye Ligi Kuu bara.
