UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI - 11

Inaandikwa na Fikiri Salum

Ilipoishia 

HIYO ilitokana na msimamo wa msingi wa urekebisho wa Kiprotestanti wa kutaka kila mmoja aweze kutafsiri Biblia alivyoielewa bila kutegemea mapokeo wala mamlaka rasmi ya kanisa, ila msaada wa roho mtakatifu 


Endelea

Umoja halisi wa kanisa unaweza kupatikana tu katika ukweli wa injili ya Yesu Kristo, ni habari mbaya kwamba katika karne ya 16 kuupigania ukweli huo kulivunja umoja wa Ukristo wa magharibi, haiwezekani kushangilia mafarakano ya wafuasi wa Yesu.

Yake ya karne hiyo yalitokana na kuelewa tofauti kweli za imani ya Kikristo na yalikuwa na ukali kwa sababu pande zote zilisadiki kwamba kushikilia kwa usahihi ufunuo wa Mungu ni suala la wokovu wa milele.

Kwa mfano Martin Luther aliandika sikubali mafundisho yangu yahukumiwe na yeyote, hata kama ni malaika, asiyekubali mafundisho yangu hawezi kufikia wokovu (11).

Pamoja na hayo, mambo mengi yalichangia farakano, si Teolojia tu bali siasa, uchumi, jamii na utamaduni, wakati huo mara nyingi hoja za imani na malengo ya kisiasa vilichanganyikana, wanasiasa wengi walitumia hoja hizo Ili kufikia malengo ya kuitawala, na vilevile wanateolojia walitumia siasa kutetea mafundisho yao Ili kuvuta watu.

Ndiyo sababu Luther alichorwa kama shujaa wa taifa la Ujerumani, mara nyingi pande zote zilipotosha maana ya wapinzani na kuwachora vibaya wakivunja amri ya nane inayokataza uongozi dhidi ya jirani.

Hata waliojitahidi kusema ukweli tu juu ya wengine kwa kawaida hawakujirahidi vya kutosha kuelewa msimamo wao na kuona kwamba pengine SI mbaya zaidi.

Kila mmoja alitaka ushindi akachangia ugomvi uliorithiwa kwa vizazi vilivyofuata, hivyo kilichosababisha zaidi farakano si masuala ya imani yaliyojadiliwa na Waprotestanti, bali lawama zao dhidi ya hali mbaya ya kanisa la wakati huo iliyokuwa inakera wengi na kuwaelekeza kuunga mkono urekebisho.

Hapo kale neno hilo (kwa Kilatini Formatio) lilihusu badiliko la hali mbaya iliyopo Ili kurudia hali nzuri zaidi ya awali.

Karne  za kati lilitumika mara nyingi marekebisho ya Umonaki, katika karne ya 15 hoja ya urekebisho ilionekana wazi si tu kwa mashirika ya Kitawa Bali kwa kanisa lote.

Hata mtaguso wa Konstanz (1414- 1418) ulidai kabisa ufanyike katika kichwa na katika viungo, lakini kwa ujumla mitaguso yote ya karne za kati na mikutano mingi ya Bunge la Dola la Kijerumani ililenga urekebisho wa kanisa.

Kwa kweli karne za kati zilikuwa na mchanganyiko wa mambo yaliyopingana ibada za nje tu na za dhati kabisa teolojia iliyoelekeza kutenda kwa msingi wa nipe nikupe na hakika ya kwamba binadamu anategemea kabisa neema ya Mungu.

INAENDELEA 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI