UKRISTO NI CHIMBUKO LA UYAHUDI - 10

Inaandikwa na Fikiri Salum

ISIPOKUWA kwa kuwaachia watawale Italia ya kati, walisababisha Papa aanze kuwa kama Mfalme wa dunia hii, jambo lililoathiri sana majukumu yake ya kiroho hadi mwaka 1870.

Endelea

Katika karne za kati Ulaya yote ilikwisha kuwa ya Kikristo, kutoka huko ilienea, pamoja na ustaarabu wa magharibi, ulioathiriwa sana na Ukristo katika Amerika yote na sehemu nyingine za dunia.

MAFARAKANO MAKUU KATI YA WAKRISTO

Katika historia ndefu ya Ukristo, yalitokea mafarakano mengi waamini wa Yesu wakizidi kutofautisha, makundi makubwa zaidi ni kanisa katoliki, Makanisa ya Waorthodoksi na ya Waorthodoksi wa mashariki na madhehebu ya Uprotestanti, hasa tangu mwaka 1910 madhehebu mengi yanashiriki juhudi za Ekumeni kwa ajili ya kurudisha umoja wa awali.

WAKATOLIKI

Zaidi ya nusu ya Wakristo wote wanashikamana katika imani na sakramenti chini ya Maaskofu wenye ushirika kamili na yule wa Roma, ambaye kwa kawaida anaitwa Papa.

Kati yao umoja unazingatiwa sana kama sifa ya kwanza ya kanisa inayotambulisha wanafunzi wa Yesu.

Neno 'katoliki' tunaendelea kulitumia zaidi kwa maana ya madhehebu maalum yenye wafuasi wengi duniani, kiteolojia linamaanisha "kanisa lililopo popote lililo moja tu kila mahari na kila wakati", kwa maana hiyo kila Mkristo yumo katika Ukatoliki, kwani mbele ya Kristo kanisa ni moja tu kila mahali duniani.

Waanglikana, Walutheri, Wamoravia na wengineo huamini kabisa kwamba wenyewe ni sehemu ya kanisa lile moja la bwana Yesu lililopo mahari popote.

Upande mwingine, hata kanisa "katoliki linaloongozwa na Askofu' (Papa) wa Roma ni la "Kiinjili", kwani linakubali na kutangaza Injili (=Habari njema) ya Yesu Kristo.

WAORTHODOKSI NA WAORTHODOKSI WA MASHARIKI

Wakristo wengi walioishi upande wa mashariki wa Dola la Kirumi na ng' ambo ya mipaka yake ya mashariki walitengana na Wakatoliki hasa katika karne ya V (Waorthodoksi wa mashariki na Karne X1 (Waorthodoksi).

Hata hivyo msimamo wa imani tofauti sana, kwa kuwa wanachanga mapokeo ya awali ya kanisa la mitume na la mababu.

WAPROTESTANTI

Utitiri wa madhehebu ya Waprotestanti ndio wenye tofauti kubwa zaidi kati yao wenyewe na kati yao na Wakristo waliotajwa kwanza.

Hiyo ilitokana na msimamo wa msingi wa urekebisho wa Kiprotestanti wa kutaka kila mmoja, aweze kutafsiri Biblia alivyoielewa, bila kutegemea mapokeo wala mamlaka rasmi ya kanisa, ila msaada wa roho mtakatifu.

INAENDELEA 


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI