Timu ya akina Kibu Denis yachapwa huko Libya

Baada ya michezo 12 kupita bila ya kupoteza mchezo wowote ule kwa timu ya Al-Nasry ndani ya group 4 la ligi kuu ya Libya msimu huu, hatimae leo wamepoteza mchezo.

Al-Nasry leo wamepoteza mchezo wao wa kwanza wa ligi kuu kwa kipigo cha mabao 2-1 dhidi ya klabu ya Al-Wafaq.

Licha ya kipigo hicho Al-Nasry bado inandelea kusalia kileleni mwa group 4 wakiwa na alama zao 31 walizozipata kwenye michezo 12 waliyocheza mpaka sasa.

Nyota wa zamani wa Simba SC, Kibu Dennis, Steven Mukwala na Fabrice Ngoma wote kwa pamoja walikuwa sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo huo.

Na hiki sasa ndicho kipigo cha kwanza cha Al-Nasry toka Kibu na Mukwala wajiunge rasmi na klabu hiyo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Beno Ngassa mdogo wa Mrisho Ngassa anayekipiga Tanzania Prisons