Abdi Banda akumbushia alivyoondoka Simba kwa mbinde
Beki Kisiki Abdi Banda anasema watu wasichojua wakati anasajiliwa kwa mara ya kwanza nchini Afrika Kusini, alisubiri barua ya Simba kumruhusu kuondoka tangu alfajiri mpaka jioni katika ofisi za klabu hiyo wakati huo zipo Posta lakini hakuipata n kesho yake ana ticket ya ndege ili kurejea nchini humo.
"Sikula kutwa nzima, baadhi ya viongozi walikuwa wakinipita tu kwenye wakati ilikuwa ni jambo dogo sana juu ya barua yangu, ilinikasirisha maana sikuwa nimefanya jambo baya, nilifuata utaratibu ila hakuna aliyenipa msaada mpaka kiongozi
Mmoja wa Simba aliyepiga simu kutoka nje ya nchi na kuahidi atafatilia hivyo naweza nikaondoka"
"Nilipofika airport, Waandishi walinihoji, sikuficha nilielezea ukweli wote sasa kusema kuwa viongozi wameninyima barua ndiyo ikawa kosa kuambiwa nimeitukana Simba"
"Embu niambie hapo kosa langu ni nini? Kusema ukweli?" Ameniambia Banda.
