Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Septemba, 2025

Licha ya kutoitwa Stars, Kelvin John aendeleza umwamba Denmark

Mabao mawili ya mshambuliaji wa Tanzania Kelvin John anayekipiga Aalborg ya Denmark yameifanya timu hiyo ifuzu hatua ya 16 Bora ya Kombe Denish Cup Sec Round. Kelvin amefunga mabao hayo katika ushindi wa mabao 6-1, huku mabao mengine yakipachikwa wavuni na Hellenius aliyefunga mabao mawili na Ross na Conilius waliofunga bao moja moja.

Police FC yaanza vema kombe la Kagame

MABINGWA wa Kenya, Polisi wameanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya kuichapa Garde Cotes FC​ya Djibouti mabao 4-0 katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. Mabao ya Polisi inayofundishwa na Kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje yamefungwa na Erick Zakayo dakika ya 19, David Simiyu dakika ya 34,Baraka Badi dakika ya 65 na Edward Omondi dakika ya 67.

Singida Black Stars yashikwa shati na Coffee ya Ethiopia

WENYEJI, Singida Black Stars wamelazimishwa sare ya bila mabao na Coffee ya Ethiopia katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. Pamoja na kucheza pungufu kufuatia kipa wao, Ibrahim Donald kutolewa kwa kadi nyekundu mapema tu, lakini Coffee walimudu kumaliza mchezo bila kupoteza. Katika mchezo wa Kundi A uliotangulia , mabingwa wa Kenya, Polisi walianza vyema michuano hiyo kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Garde Cotes FC​ya Djibouti mabao 4-0 hapo hapo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo. Mabao ya Polisi inayofundishwa na Kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje yamefungwa na Erick Zakayo dakika ya 19, David Simiyu dakika ya 34,Baraka Badi dakika ya 65 na Edward Omondi dakika ya 67.

Wachezaji Stars waingia kambini

WACHEZAJI wa timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’ wameingia kambini leo Jijini Dar es Salaam tayari kwa safari kwenda Jijini Brazaville, Kongo kesho kwa ajili ya mchezo wa Kundi E kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2026. Taifa Stars inatarajiwa kucheza na Kongo-Brazzaville Septemba 5 Uwanja wa Stade Alphonse Massemba-Débat Jijini Brazzaville kuwania tiketi ya Fainali za Kombe la Dunia 2026 zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Canada, Mexico na Marekani. Baada ya hapo, Taifa Stars itarejea nyumbani kwa ajili ya mchezo mwingine wa kundi hilo kufuzu Kombe la Dunia dhidi ya Niger Septemba 9 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Taifa Stars inashika nafasi ya pili kwenye Kundi E kwa pointi zake tisa, nyuma ya Morocco inayoongoza kwa pointi zake 15, wakati Kongo ambayo haina pointi inashika mkia baada ya timu zote kucheza mechi tano. Kwa upande wao Niger wanashika nafasi ya nne kwa pointi zao sita za mechi nne nyuma ya Zambia yenye pointi sita pia za mechi tano. Timu tisa zitakazoongoza ma...

Msigwa azipiga mkwara Yanga na Simba

Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo Gerson Msigwa ametoa tahadhari kwa vilabu vya Simba na Yanga kuhusu matumizi ya Uwanja wa Benjamin Mkapa. . "Wote ambao mmeomba kutumia uwanja wa Benjamin Mkapa (Simba na Yanga) tunaomba tuelewane tutakapowaambia tafuteni uwanja mwingine, kwa sababu tunataka tufanye ukarabati, itakapofika hapo isiwe mgogoro" . -Mhe Gerson Msigwa, Msemaji Mkuu wa Serikali na Katibu Mkuu wa Wizara ya Sanaa, Utamaduni na Michezo.

Fadlu David's aipigia magoti Jayruthy

“Yanga wana Wachezaji wakubwa kwa ajili ya mechi kubwa, nasi tunahitaji aina hiyo ya Wachezaji ili kupambana nao kwanza nimpongeze Rais MO Dewji kwa usajili mzuri ila nataraji Jayrutty atatusaidia Mchezaji mmoja mwenye utofauti katika eneo la mwisho, hata msimu uliyopita tulipata changamoto mechi kubwa fainali ya Shirikisho na hata dhidi ya Yanga kwasasabu tulikosa aina hiyo ya Mchezaji katika eneo la mwisho, kabla dirisha halijafungwa natamani sana tumpate Mchezaji wa aina hii” Anasema Fadlu Davids kupitia Azam TV.

Alikamwe atambia Yanga Princess

“Tutakuwa na mchezo wa timu ya Yanga Princess siku ya Kilele cha 𝐖𝐢𝐤𝐢 𝐲𝐚 𝐌𝐰𝐚𝐧𝐚𝐧𝐜𝐡𝐢, Yanga Princess msimu huu ni moja kati ya timu ambayo tumefanya usajili bora sana. Tumeonesha jeuri ya fedha. Tumemrejesha Precious, Wincate na Mynaco.  Tumehakikisha wachezaji wetu bora kama akina Aregash wamesalia. Mratibu wa Yanga Princess amesema hakuna tena kisingizio” “Tutakuwa na mchezo mwingine muhimu sana wa timu ya viongozi wa Yanga na wasanii, huu utakuwa mchezo wa kukata na shoka.  Mechi ya mwisho nilitokea benchi ila mchezo huu nitakwenda kuanza na wasipokuwa makini nitachukua na kitambaa kabisa. Kocha wetu Romain Folz na msaidizi wake Rodriguez nao watakuwepo”

Kocha Taifa Stars awaangukia Waandishi wa Tanzania

Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Hemed Suleiman amemuombea radhi Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo Julio kwa kauli aliyoitoa. Julio alinukuliwa akisema kuwa “Waandishi wana roho mbaya” hii ni baada ya kufanyika Mkutano wa Makocha na Waandishi Habari jana na mahudhurio ya Waandishi kuwa machache kiasi cha kuwatuhumu kuwa sio Wazalendo. “Mimi siwezi kumsemea Julio yeye atalitatua lake ila mimi nilikuwa namaanisha kitu kimoja, sidhani kama Waandishi wa habari wana roho mbaya mimi namaanisha kuhudhuria kwao kwenye zile press (Za Taifa Stars) wamekuwa wachache” “Mpira wa Tanzania unahitaji Waandishi ili kuweza kuufikisha pale ambapo unatakiwa ufike, ninachukua pia nafasi hii kumuombea msamaha (Julio) nafikiri amekosea”

Yanga Princess kutambulisha Mdhamini wake wa jezi

Uongozi w klabu ya Yanga SC upo mbioni kumtambulisha mdhamini wao mpya ambaye atavaliwa kwenye jezi za kikosi cha Yanga Princess, Misimu yote ya nyuma walikuwa wakivaa jezi zenye mdhamini sawa na timu yao ya kiume ambaye ni Sportpesa ila msimu huu mpya itakuwa tofauti kidogo kwa maana na wao Yanga Princess watakuwa na mdhamini wao tofauti na Sportpesa.

Balla Moussa Conte kwenye timu ya taifa

Kiungo wa Yanga SC Moussa Balla Conte kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa ya Guinea. Guinea watacheza dhidi ya Somalia na Algeria kwenye mechi za kufuzu World Cup 2026.

Mwandishi wa Ghana aimwagia sifa CHAN ya mwaka huu

MWANDISHI wa Habari wa Ghana Soccernet, Nuhu Adam amesema Michuano ya Mataifa ya Afrika kwa wachezaji wa Ligi za Ndani (CHAN 2024), iliyofanyika Tanzania, Kenya na Uganda ndiyo bora zaidi kwake tangu imeanza rasmi mwaka 2009. "Hii ni hatua nzuri kwa nchi zote tatu ambazo zimeandaa michuano hii, nafikiri kwangu ndiyo mashindano bora zaidi kuwahi kutokea, CAF ilifanya kazi yake vizuri kwa kushirikiana na wenyeji, hivyo kiukweli ni jambo la kuvutia," amesema Nuhu. Nuhu amesema sababu ya Shirikisho la Soka Africa (CAF), kuanzisha CHAN ni dalili nzuri ya kuandaa vizuri timu zote za ukanda wa Afrika kwa ajili ya kujiandaa na michuano ya AFCON, ambayo ndio mikubwa zaidi kutokana na aina ya wachezaji. "Siwezi kuzungumzia kasoro kwa sababu yapo mambo mengi yamefanyika kwa soka la Afrika Mashariki, timu kama Yanga, Simba kwa Tanzania, Gor Mahia ya Kenya zinafanya vizuri pia, hii ni dalili tosha ya jinsi nchi hizo tatu zilivyopiga hatua." Aidha, Nuhu amesema licha ya maandaliz...

Kelvin John aliliwa Taifa Stars

KELVIN John akiwa na Aalborg FC msimu huu tayari amepachika Mabao matatu kwenye michezo 8 waliyocheza huku akiwa mchezaji tegemezi kwenye Kikosi hicho  Kelvin ana wastani wa kucheza dakika 88 kwenye kila mchezo (kwenye michezo 8 waliyocheza Hadi hivi sasa) Ila hizi takwimu hazijatosha kumfanya @kelvin.p.john aitwe timu ya Taifa isipokuwa kaitwa Selemani Mwalimu (pia ni mchezaji mzuri sana) ambaye hakuwa na game time ya kutosha pale Wydad AC na hata takwimu zake hazireflect sana 

Kocha wa Yanga hali tete Misri

Aliyewahi kuwa kocha mkuu wa klabu ya Yanga ambaye kwasasa ni kocha mkuu wa klabu ya Ismailia inayoshiriki ligi kuu ya Misri Miloud Hamdi’s anashika mkia kwenye ligi Egyptian Premier League baada ya kucheza michezo mitano na kuambilia sare mbili pekee. Klabu hiyo ya ipo nafasi ya 20 baada ya mechi tano na tofauti ya magoli ya kufunga na kufingwa hadi sasa ikiwa ni -6

Kipa Simba atimkia kwao

Golikipa wa Klabu ya Simba SC,  Moussa Camara ameanza safari ya kuelekea nchini kwao Guinea kwaajili ya kujiunga na na Kikosi cha timu ya Taifa ya Guinea  kitakachocheza michezo miwili ya kufuzu ambapo Septemba 5 kitacheza dhidi ya Somalia nchini Uganda na Septemba 8 dhidi ya Algeria nchini Morocco.

Hemed Morocco alia na Waandishi wa Tanzania

Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars , Hemed Morocco amewashurumi Wanahabari wa Tanzania kwa kushindwa kuonesha uzalendo kwa timu yao ya taifa ilipokuwa inashiriki kombe la CHAN. "Najisikia vibaya na waandishi wa habari wa kwetu wameshindwa kuwa wazalendo na timu ya Taifa, tunaona waandishi wa nchi nyingine walivyo wazalendo na nchi zao, Waandishi wanapaswa kuisapoti timu yao, wanapaswa kuja kwenye interview." Mimi kama Kocha wa Taifa Stars nawaomba sana waandishi waisapoti timu yao maana hata wakitusema sisi tutachukulia kama changamoto ya kutusukuma ila mueneshe tu uzalendo kwa timu ya taifa kwa kijitokeza kwa wingi, mfano kama hapa mmekuja wachache ila mlipaswa kuwa wengi kuonesha tu kuwa mnaisapoti timu ya taifa lenu. Sisi tunasafiri sana huko tunaona namna waandishi wanajitokeza kwenye mahojiano ama press za timu zao zinapocheza wao wanaenda kwa wingi ishara ya Uzalendo ila kwetu waandishi wamekosa uzalendo kabisa, kwa nyie wachache mliokuja nawaomba sana muhahimize ...