Kocha mkuu wa timu ya taifa, Taifa Stars , Hemed Morocco amewashurumi Wanahabari wa Tanzania kwa kushindwa kuonesha uzalendo kwa timu yao ya taifa ilipokuwa inashiriki kombe la CHAN.
"Najisikia vibaya na waandishi wa habari wa kwetu wameshindwa kuwa wazalendo na timu ya Taifa, tunaona waandishi wa nchi nyingine walivyo wazalendo na nchi zao, Waandishi wanapaswa kuisapoti timu yao, wanapaswa kuja kwenye interview."
Mimi kama Kocha wa Taifa Stars nawaomba sana waandishi waisapoti timu yao maana hata wakitusema sisi tutachukulia kama changamoto ya kutusukuma ila mueneshe tu uzalendo kwa timu ya taifa kwa kijitokeza kwa wingi, mfano kama hapa mmekuja wachache ila mlipaswa kuwa wengi kuonesha tu kuwa mnaisapoti timu ya taifa lenu.
Sisi tunasafiri sana huko tunaona namna waandishi wanajitokeza kwenye mahojiano ama press za timu zao zinapocheza wao wanaenda kwa wingi ishara ya Uzalendo ila kwetu waandishi wamekosa uzalendo kabisa, kwa nyie wachache mliokuja nawaomba sana muhahimize waandishi wengine waje sisi hata wakitukosoa tunachukulia kama changamoto ila uwepo wao ni muhimu sana kama uzalendo kwa taifa lao."
- Hemed Morocco
Kocha Mkuu wa Taifa Stars.