WENYEJI, Singida Black Stars wamelazimishwa sare ya bila mabao na Coffee ya Ethiopia katika mchezo wa ufunguzi wa Kundi A michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame jioni ya leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Pamoja na kucheza pungufu kufuatia kipa wao, Ibrahim Donald kutolewa kwa kadi nyekundu mapema tu, lakini Coffee walimudu kumaliza mchezo bila kupoteza.
Katika mchezo wa Kundi A uliotangulia , mabingwa wa Kenya, Polisi walianza vyema michuano hiyo kwa ushindi wa 4-0 dhidi ya Garde Cotes FCya Djibouti mabao 4-0 hapo hapo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo.
Mabao ya Polisi inayofundishwa na Kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje yamefungwa na Erick Zakayo dakika ya 19, David Simiyu dakika ya 34,Baraka Badi dakika ya 65 na Edward Omondi dakika ya 67.