Kocha Mkuu wa Timu ya Taifa ya Tanzania Taifa Stars Hemed Suleiman amemuombea radhi Msaidizi wake Jamhuri Kihwelo Julio kwa kauli aliyoitoa.
Julio alinukuliwa akisema kuwa “Waandishi wana roho mbaya” hii ni baada ya kufanyika Mkutano wa Makocha na Waandishi Habari jana na mahudhurio ya Waandishi kuwa machache kiasi cha kuwatuhumu kuwa sio Wazalendo.
“Mimi siwezi kumsemea Julio yeye atalitatua lake ila mimi nilikuwa namaanisha kitu kimoja, sidhani kama Waandishi wa habari wana roho mbaya mimi namaanisha kuhudhuria kwao kwenye zile press (Za Taifa Stars) wamekuwa wachache”
“Mpira wa Tanzania unahitaji Waandishi ili kuweza kuufikisha pale ambapo unatakiwa ufike, ninachukua pia nafasi hii kumuombea msamaha (Julio) nafikiri amekosea”