MABINGWA wa Kenya, Polisi wameanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya kuichapa Garde Cotes FCya Djibouti mabao 4-0 katika mchezo wa Kundi A leo Uwanja wa Meja Jenerali Charles Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam.
Mabao ya Polisi inayofundishwa na Kocha Mrundi, Etienne Ndayiragijje yamefungwa na Erick Zakayo dakika ya 19, David Simiyu dakika ya 34,Baraka Badi dakika ya 65 na Edward Omondi dakika ya 67.