Mabao mawili ya mshambuliaji wa Tanzania Kelvin John anayekipiga Aalborg ya Denmark yameifanya timu hiyo ifuzu hatua ya 16 Bora ya Kombe Denish Cup Sec Round.
Kelvin amefunga mabao hayo katika ushindi wa mabao 6-1, huku mabao mengine yakipachikwa wavuni na Hellenius aliyefunga mabao mawili na Ross na Conilius waliofunga bao moja moja.