Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Kispoti

Yanga wapo katika wakati mgumu lakini........

Na Prince Hoza

TANGU alipojiondoa Yusuf Mehbood Manji ambaye alikuwa mwenyekiti na mfadhili wa klabu ya Yanga morali imeshuka, fedha imetoweka hata kasi ya timu inaonekana kupungua.

Uwepo wa Manji ndani ya Yanga uliwapa faida kubwa Wanayanga, Yanga imetawala soka la Tanzania takribani miaka mitano, huku ikiwateza mahasimu wao Simba Sc ambao ilifikia wakati ilipachikwa jina la utani la "Wamchangani" jina ambalo walibatizwa na aliyekuwa msemaji wa Yanga, Jerry Muro.

Jerry Muro akaendelea kuibatiza majina mengine ya utani Simba na kuwakera mashabiki wake, Simba iliitwa "Wamatopeni" na hiyo yote ni kutokana na matokeo mabovu iliyopata.

Uwepo wa Manji uliwafanya wachezaji wa Yanga waishi kifalme, Yanga iliweza kusajili wachezaji bora kutoka kila mahari, na ndio maana ikaweza kujiwekea historia ya kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara mara tatu mfululizo.

Manji akaipoteza kabisa Simba ambayo ilishindwa kufurukuta na kukosa taji la Ligi Kuu misimu minne mfululizo, Simba ikapotea kabisa kwenye anga za kimataifa na imerejea mwaka huu hasa baada ya Manji kuondoka Yanga.

Ina maana Manji angeendelea Yanga, Simba isingefurukuta, jeuri ya Manji iliweza kuibomoa Simba hasa akifanikiwa kuwasajili wachezaji muhimu wa Wekundu hao wa Msimhazi, Yanga iliwanasa nyota kama Kevin Yondan, Ally Mustapha "Barthez", Hassan Kessy, Mbuyu Twite, Amissi Tambwe, Emmanuel Okwi na wengineo.

Mastaa wa Yanga waliendelea kusalia kikosini, hakuna timu iliyokuwa na ubavu wa kuweza kuwatikisa, Yanga ilitambia nyota wake kama Wazimbabwe, Donald Ngoma, Thabani Kamusoko, Mrundi, Amissi Tambwe ambaye amekuwa mfungaji bora, Simon Msuva, Vincent Bossou raia wa Togo na wengineo.

Kwa bahati mbaya Manji akajiondoa Yanga, sitaki kuzungumzia kilichomuondoa nisije nikajikuta sentro, ila maisha ya Yanga yamebadilika sana si kwa wachezaji, viongozi na mashabiki.

Morali ya wachezaji imeshuka mno, Yanga iliyokuwa na pesa lukuki za Manji ilifikia hatua ikaajili makocha wanne, wawili kati yao ni bora barani Afrika, ambao ni Mholanzi, Hans Van der Pluijm aliyegeuzwa kuwa mkurugenzi wa ufundi na Mzambia George Lwandamina, kocha mkuu, Juma Mwambusi kocha msaidizi na Mzambia, Noel Mwandila pia msaidizi.

Yanga ikaanza kuyumba alipojiondoa Manji, wachezaji mastaa wakaanza kugoma, kwa mfano Donald Ngoma na Vincent Bossou, Ngoma raia wa Zimbabwe na Bossou raia wa Togo wakagoma kucheza kushinikiza kulipwa stahiki zao, kwani uongozi wa sasa wa Yanga umewataka wacheze kwa kujitolea kwakuwa fedha hakuna, Haruna Nuyonzima akaona isiwe shida akasepa zake, Bossou naye akatimka, amebaki Ngoma na kuendeleza mgomo wake ingawa akisai ni mgonjwa.

Pia tumeona wachezaji kama Beno Kakolanya, Obrey Chirwa raia wa Zambua nao wakiendeleza mgomo baridi wakitaka walipwe fedha zao za usajili pamoja na mishahara.

Ni kweli hiyo ni haki yao kudai fedha zao kwani maisha yao wanategemea soka pekee, ukiangalia hata upambanaji wa Yanga uwanjani umeshuka mno, Yanga hata inapokutana na timu isiyo na ushindani lakini kwao mechi inakuwa ngumu.

Na kwenye msimamo wa ligi Yanga inakamata nafasi ya pili ikiwa nyuma ya mahasimu wao Simba Sc wanaoongoza kwa pointi 42 huku Yanga wakiwa na pointi 37 zikiwa ni tofauti ya pointi tano, lakini kuna utofauti mkubwa kati ya Yanga na mahasimu wao Simba.

Simba kwa sasa wana morali ya juu kwakuwa pesa ipo hasa baada ya mwanachama wao mfanyabiashara mkubwa hapa nchini, Mohamed Dewji "Mo" kujitokeza kuisaidia.

Mo mbali na kushinda zabuni ya kuimiliki Simba iliyongia kwenye mfumo wa kuuza Hisa, amekuwa akijitolea fedha zake kwa ajili ya usajili na maradhi, kitu ambacho kimewafanya Simba kupata kikosi bora na hatari msimu huu.

Simba imetengeneza kikosi chenye mastaa kama Emmanuel Okwi raia wa Uganda, James Kotei na Asante Kwasi raia wa Ghana, John Bocco "Adebayor", Shiza Kichuya, Said Ndemla, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe na Aishi Manula ambao wanaipa jeuri Simba kwa sasa.

Lakini Yanga mbali na kuishiwa fedha bado wanapambana na hali yao, Yanga na umasikini wao wamefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya Azam Sports Federation Cup kwa kuichakaza Majimaji ya Songea mabao 2-1 jana jioni.

Yanga na umasikini wametinga raundi ya pili ya Ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuitoa mashindanoni Saint Louis ya Shelisheli kwa jumla ya mabao 2-1, ikishinda 1-0 nyumbani na ikilazimisha sare ya 1-1 ugenini, Yanga na umasikini wao bado wanaifukuzia Simba kileleni mwa Ligi Kuu Bara.

Yanga hiyo hiyo isiyo na pesa bado inapambana katika kipindi kigumu kwani karibu wachezaji wake wa kikosi cha kwanza ni majeruhi kiasi kwamba inalazimika kutumia wachezaji wake wa akiba na wanaibeba timu, tofauti na mahasimu wao Simba ambao wao licha ya kuongoza ligi na kutinga raundi ya pili kombe la Shirikisho barani Afrika, lakini wametolewa mapema kwenye kombe la Azam Sports Federation Cup hivyo inawapa wakati mgumu mwakani kushiriki michuano ya kimataifa kama wataukosa ubingwa wa bara

Alamsiki

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...