SIMBA KANYAGA TWENDE HADI UBINGWA

Na Ikram Khamees. Dar es Salaam

Vinara wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Simba Sc, jioni ya leo wameendeleza ubabe wao baada ya kuichapa bila huruma Mbao Fc ya Mwanza mabao 5-0 uwanja wa Taifa mjini Dar es Salaam.

Mbao Fc walionekana kuibana Simba dakika 20 za mwanzo wa mchezo lakini kocha wa Simba aliona udhaifu wa Simba na kuamua kumwingiza kiungo Mzamiru Yassin ambaye akaubadili mchezo na Simba kuanza kujipatia mabao mawili hadi mapumziko.

Shiza Kichuya alianza kufunga dakika ya 38 kabla ya Emmanuel Okwi ajaongeza la pili dakika ya 41, kipindi cha pili Okwi tena akafunga la tatu dakika ya 68 wakati Erasto Nyoni akafunga la nne na Mghana, Nicolaus Gyan alihitimisha kalamu ya magoli kwa kufunga dakika ya 86.

Kwa matokeo hayo Simba wanafikisha pointi 45 wakiendelea kuongoza na sasa ikitanua gepu kubwa na mahasimu wao Yanga ambao wanafuatia kwa kushika nafasi ya pili, Yanga ina pointi 37 ikiachwa nyuma kwa pointi 7

Simba imeifunga Mbao mabao 5-0

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

STAA WETU: JEREMIA JUMA MTOTO WA JUMA MGUNDA ALIYEIKACHA SIMBA NA KUENDELEA NA UASKARI