Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Mei, 2025

Huyu jamaa Frank Assinki aliupiga kazi nzuri sana leo

Huyu jamaa Frank Assinki amepiga kazi sana amewapika sana washambuliaji wa Simba vya kutosha! Kuna beki mzuri sana ndani yake. Ule utulivu na zile decision making ni za kiwango cha juu sana! Katika mita 20 za mwisho za Singida Black Stars alivuja jasho vya kutosha kwa kila nyasi! Best best defender. Alikuwa na game nzuri sana yaani alikuwa anahesabu tu wanaokuja kushambulia ) Yani dira yangu imenasa kwake, amenipa nafasi ya kumtazama zaidi katika game zijazo hasa hasa next season.. Singida Black Stars wamepata faida sana kumiliki beki wa kati wa namna hii! Football yake nzuri sana.

Petro de Luanda yamtema straika wake mkongwe

Klabu ya Petro de Luanda wameachana rasmi na mshambuliaji wao mkongwe Adriano Nicolau, maarufu kwa jina la Yano. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alirejea klabuni katikati mwa msimu wa 2024/25, na kucheza mechi 11 bila kufunga bao hata moja.

Singida Black Stars yaifuata Yanga fainali ya kombe la CRDB

TIMU ya Singida Black Stars imefanikiwa kwenda Fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), michuano inayodhaminiwa na Benki ya CRDB baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Simba SC jioni ya leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa, Babati mkoani Manyara. Mabao yote ya Singida Black Stars yamefungwa na wachezaji kutoka Ghana, mshambuliaji Mghana, Jonathan Sowah dakika ya 17 na kiungo Emmanuel Kwame Keyekeh mawili dakika ya 35 na 48, wakati bao pekee la Simba SC limefungwa na kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 49. Bao la kwanza langoni alikuwa kipa Mguinea, Moussa ‘Pin Pin’ Camara, lakini akatoka nje dakika ya 25 baada ya kuumia kufuatia kugongana na Sowah – nafasi yake ikachukuliwa Ally Salim aliyeruhusu mabao mengine mawili ya Kayekeh.

Yanga yashikilia msimamo wake, hawachezi dabi

Bodi ya Ligi Kuu nchini Tanzania TPLB siku ya Jana ilifanya mawasiliano na Uongozi wa juu wa klabu ya Young Africans Sports Club kujadili masuala mbalimbali kuhusu mechi zilizosalia za kumaliza msimu. Uongozi wa klabu ya Young Africans Sports Club đź”° umeshikilia msimamo ule ule wa kusema hawautambui Mchezo wa tarehe 15/06/2025,wanatambua michezo miwili ya Ligi kuu ndio wamebakiza wao na Mchezo mmoja wa Fainali ya FA basi na si michezo mingine. Mpaka kufikia Sasa hakuna muafaka wowote uliofikiwa baina ya pande hizo mbili kuhusu kutatua kitendawili Cha Mchezo huo ambao uliahiriahwa tarehe 08/03/2025 bila kufuatwa kwa kanuni. Mazungumzo Bado yanaendelea ikishirikisha Viongozi wa Serikali pia

Stars ya kushiriki COSAFA hadharani

Kikosi cha Taifa Stars kitakachoingia kambini Juni 2,2025 kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Afrika Kusini (Bafana Bafana) na mashindano ya COSAFA dhidi ya Eswatini na Madagascar. Katika kikosi hicho majina mapya ni Yacouba Seleman na Wilson Nangu wote wa JKT Tanzania ambao wametokea kufanya vizuri katika siku za karibuni

Tshabalala kuongeza miaka miwili Simba

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka vyanzo vya kuaminika, Mwamuzi wa Kimataifa kutoka Tanzania, Ahmed Arajiga, ameteuliwa rasmi kuchezesha mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la CRDB (CRDB Federation Cup) kati ya miamba wa soka la Tanzania, Simba SC na Singida Black Stars. Mchezo huo wa kusisimua unatarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Tanzanite (Kwara), ukiwa ni moja ya mechi ngumu na za kuvutia zaidi kwenye ratiba ya msimu huu wa michuano ya CRDB. Kuteuliwa kwa Arajiga kuamua mchezo huu ni uthibitisho wa kuaminiwa kwa muamuzi huyo kwenye mechi za presha na zenye mvutano mkubwa. Simba SC wanaingia wakiwa na rekodi ya mafanikio katika michuano hii, huku Singida Black Stars wakisaka nafasi ya kuandika historia kwa mara ya kwanza. Mchezo huu utatoa mshindi atakayekutana na Yanga SC kwenye Fainali ya Kombe la CRDB, baada ya Yanga kufuzu mapema na kuweka rekodi ya kufika fainali nyingine tena mfululizo.

Arajiga kuchezesha Simba na Singida Black Stars nusu fainali kesho

Kwa mujibu wa taarifa za ndani kutoka vyanzo vya kuaminika, Mwamuzi wa Kimataifa kutoka Tanzania, Ahmed Arajiga, ameteuliwa rasmi kuchezesha mchezo wa Nusu Fainali ya Kombe la CRDB (CRDB Federation Cup) kati ya miamba wa soka la Tanzania, Simba SC na Singida Black Stars. Mchezo huo wa kusisimua unatarajiwa kupigwa kesho kwenye Uwanja wa Tanzanite (Kwara), ukiwa ni moja ya mechi ngumu na za kuvutia zaidi kwenye ratiba ya msimu huu wa michuano ya CRDB. Kuteuliwa kwa Arajiga kuamua mchezo huu ni uthibitisho wa kuaminiwa kwa muamuzi huyo kwenye mechi za presha na zenye mvutano mkubwa. Simba SC wanaingia wakiwa na rekodi ya mafanikio katika michuano hii, huku Singida Black Stars wakisaka nafasi ya kuandika historia kwa mara ya kwanza. Mchezo huu utatoa mshindi atakayekutana na Yanga SC kwenye Fainali ya Kombe la CRDB, baada ya Yanga kufuzu mapema na kuweka rekodi ya kufika fainali nyingine tena mfululizo.

Aziz Ki, Mwalimu wapiga zoezi la mwisho kabla kuivaa FC Porto

Kiungo Mshambuliaji, Stephanie Aziz Ki pamoja na Mshambuliaji, Seleman Mwalimu wakiwa kwenye mazoezi ya mwisho ya Wydad Casablanca kabla ya kuikabili FC Porto hapo kesho. Aziz Ki atakuwa sehemu ya mchezo huo baada ya kuikosa Sevilla Mei 27.

Hiki hapa kilichomtoa Matty kwenye Dunia

Baada ya msanii Matilda au Matty kutoonekana kwenye series ya Dunia, na kuzua sintofahamu huku wengi wakidai kwamba msanii huyo anaumwa na amelazwa. Mambo Uwanjani Blog inawajuza wadau wake kwamba taarifa iliyowahi kutolewa na blogu hii kwamba Matilda hatoonekana kwenye series hiyo ni za kweli na sasa hayupo kwenye Dunia. Msanii huyo hata kama anaumwa au aumwi, lakini kilichomuondoa kwenye series hiyo ni kwamba mume anayetaka kumuoa ama mchumba wake hataki kuona mkewe au mchumba wake akiendelea na sanaa. Wadau wa Dunia wanatakiwa kuwa wavumilivu na wakubali matokeo kwamba Matilda au Matty si msanii Tena kwenye series hiyo maarufu kwasasa.

Wakala wa Feitoto aikataa Yanga

Jasmine Razack, mtaalamu wa masuala ya sheria katika michezo na msimamizi wa mchezaji Feisal Salum, amekanusha Vikali Madai ya Yanga Kwamba Watalipwa endapo mchezaji huyo atauzwa, ndani au nje ya nchi. : Yasmin ameeleza kuwa taarifa hizo ni za kupotosha na hazina msingi wowote wa kisheria, huku akisisitiza kuwa hakuna kipengele kama hicho katika makubaliano kati ya Feisal na Azam FC. : “Napenda kuweka wazi kuwa hakuna mkataba unaosema Yanga watalipwa chochote kama Feisal atauzwa. Hizo ni propaganda zisizo na ukweli wowote. Tushamvumilia sana mtu akae na uvumi huu. Sasa tunalazimika kusema ili kulinda heshima ya mchezaji,” alisema Jasmine kwa msisitizo. : Kwa siku kadhaa sasa, mitandao ya kijamii imejaa taarifa zinazodai kuwa Yanga walijihakikishia asilimia 25 ya mauzo ya Feisal endapo atauzwa nje ya nchi, au fidia ya shilingi Bilioni Moja iwapo atauzwa ndani ya ligi ya Tanzania jambo ambalo limeibua mjadala mkubwa miongoni mwa wadau wa soka. : Jasmine amesema ni muhimu kwa watu kutoa t...

Rasmi, kocha wa Orlando atambulishwa Al Ahly

KOCHA Mspaniola, JosĂ© Luis Riveiro jana alitambulishwa kuwa Kocha mpya wa Al Ahly ya Misri wiki mbili tu baada ya kuondoka Orlando Pirates ya Afrika Kusini. Mara moja Riveiro anapewa jukumu la kwenda kuiongoza Al Ahly katika michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA inayotarajiwa kufanyika nchini Marekani hivi karibuni. Ahly, kati ya wawakilishi wenne wa Afrika pamoja na Wydad Athletics ya Morocco, Esparence ya Tunisia na Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini – ipo Kundi A pamoja na wenyeji, Inter Miami, Palmeiras ya Brazil na FC Porto ya Ureno.

FIFA yakomaa na ubaguzi

Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limepitisha maazimio mapya 3 yanayohusu masuala ya ubaguzi kwenye mpira wa miguu. Maazimio hayo ni kama yafuatayo: - Mchezaji ambae atafanyiwa ubaguzi wa aina yoyote kama vile, ubaguzi wa rangi,ubaguzi wa kiraia,jinsia n.k atatakiwa kumpa taarifa mwamuzi wa mchezo husika,Kisha mwamuzi huyo atasimamisha Mchezo huo au kusitisha moja kwa moja na timu zote kuondolewa kwenye pitch. - Klabu ambayo mashabiki wake, Viongozi wake, wachezaji wake,kama watakuwa wamehusika kwenye tukio lolote la ubaguzi kwa mara ya kwanza kuanzia maazimio haya yaanze kufanya kazi,watatozwa faini yenye kiasi Cha $6M. - Endapo klabu yoyote itarudia zaidi ya mara moja kuhusika kwenye kesi za ubaguzi wa aina yoyote Ile klabu hiyo,itakumbana na adhabu moja kati ya hizi 3 au zote Kwa pamoja: *Kuzuiwa kuingiza mashabiki kwenye mechi za nyumbani zote zilizosalia. *kukatwa alama kutoka kwenye msimamo wa mashindano husika. *Kufutiwa leseni ya kushiriki kwenye mashindano husika,pamoj...

Timu 5 Ligi Kuu bara zatishia kugomea mpaka Bodi ya Ligi itoe maelezo juu ya waamuzi kuboronga

Timu tano za ligi kuu zimetishia kugomea na kutocheza mechi mbili za mwisho za NBC Premier League,mpaka pale Bodi ya ligi watakapotoa majibu ya kueleweka kutokana na matukio ya waamuzi yanayo endelea. Tayari baadhi ya timu zimeandika barua kwenda bodi ya ligi ili kupewa majibu ya kina. Hali inazidi kuwa mbaya kwenye ligi yetu

Wazee Yanga wamjibu Mguto

Kufuatia kauli aliyoitoa mwenyekiti wa Bodi ya Ligi Ndugu Steven Mguto kuhusu sakata la dabi, alisema kuwa tarehe ya Dabi ipo pale pale na kusisitiza kuwa hiyo kauli ya "HATUCHEZI" wao kama Bodi haiwezi kubadili maamuzi waliyoyapanga. Kamati ya WAZEE wa Yanga kupitia kwa Mwenyekiti wa Baraza hilo Mohammed Msumi amesema "Sisi Yanga hatuna shida na mtu yoyote lakini tunasisitiza kuwa HATUTASHIRIKI MCHEZO WA DABI hiyo Tarehe 15 mpaka haki ipatikane" "Kwanza watujibu hoja zetu 3 ,ili suluhu ipatikane, Vinginevyo hakuna kiongozi yoyote anaweza kutuamrisha,haijalishi ni kiongozi wa Bodi au wa serikali" "Kuhusu kikosi chetu hatuna wasiwasi wowote na wala hatuwaogopi Simba kwasababu tumewafunga mara 4 mfululizo" "Tunachotaka Sheria na kanuni zilizowekwa zisimamiwe ,na kama wao Bodi ya Ligi ndiyo wamekosea basi watoke Hadharani kuuomba umma radhi" MOHAMMED MSUMI M/kiti Baraza la Wazee Young Africans SC

Al Ahly mabingwa Misri

TIMU ya Al Ahly imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Misri kwa mara ya 45 baada ya ushindi wa mabao 6-0dhidi ya Pharco FC Uwanja wa Cairo International Jijini Cairo. Ilikuwa siku nzuri kwa mshambuliaji wa Kimataifa wa Palestina, Wessam Abou Ali aliyefunga mabao manne katika mchezoo huo dakika za 10, 33, 61 na 66, huku mabao mengine yakifungw ana Hussein El Shahat dakika ya 75 na Emam Ashour dakiika ya 90’+3. Ushindi huo umeifanya Al Ahly kumaliza msimu ikiwa na pointi 58, mbili zaidi ya Pyramids FC, ambao waliilaza Ceramica Cleopatra mabao 5-1 lakini wakaambulia patupu. Mashetani Wekundu walianza msimu huu chini ya Marcel Koller, lakini ni kocha wa muda Emad El-Nahhas ambaye aliwaongoza hadi hatua ya mwisho, na kupata ushindi mara sita mfululizo na akitumia mwanya wa kuteleza kwa Pyramids kutwaa taji hilo.

FADLU ANASAIDIWA NA MAREFA

Na Prince Hoza KITENDO cha Wekundu wa Msimhazi, Simba SC kutinga hatua ya fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika, sifa kemkem zinaelekezwa kwa kocha mkuu wa timu hiyo Fadlu David's raia wa Afrika Kusini. Imepita miaka 32 Simba kuingia fainali ya michuano ya CAF, ilifanya hivyo mwaka 1993 ilipofanikiwa kuingia fainali ya kombe la CAF ambalo sasa ni Shirikisho, likiunganishwa mwaka 2004 na kombe la Washindi. Simba ilikutana na timu ya Stella Abidjan ya Ivory Coast ambapo katika mchezo wa kwanza uliofanyika Ivory Coast timu hizo mbili zilitoshana nguvu kwa kutoka sare isiyo na mabao 0-0. Mchezo wa pili wa fainali uliofanyika uwanja wa Taifa, sasa Uhuru jijini Dar es Salaam na Simba ilifungwa mabao 2-0 mbele ya mgeni wa heshima, Rais wa awamu ya pili wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Alhaj Ali Hassan Mwinyi. Imepita miaka 32, Simba imerudia historia yake na ikifanikiwa kuingia fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika ambapo imekutana na timu ya RS Berkane ya Morocco, Simba ...

Nabi kaja kutalii nchini si kumfuata Feitoto

Ujio wa kocha Nasredine Nabi ndani ya Tanzania hauhusiani chochote na sakata la Usajili wa mchezaji Feisal Salum, kama nilivyoeleza majuma kadhaa nyuma. Hakuna mawasiliano ya moja kwa moja baina ya Kaizer Chiefs na Azam FC juu ya usajili wa Feitoto, Nabi hahusiki na usajili wa Kaizer Chiefs akishapendekeza jina la mchezaji kazi inafanywa na uongozi wa klabu. Feisal ana mkataba na Azam Fc, na mpaka sasa timu inayoonekana iko serious na deal ya Feisal ni Yanga nyengine zinabaki kuwa tetesi tu.

Anaandika Hans Raphael

Heri Sasii kaimaliza mechi kwa mikono yake mwenyewe Amefanya maamuzi manne makubwa ya hovyo ambayo yamezalisha matokeo ya 1-0. 1. Chamou Karaboue Alistahili kadi ya njano na Singida kupata panalty baada ya madhambi kufanyika ndani ya Box la Simba. 2. Kelvin Nashon alistahili kadi ya pili ya njano kabla ya kipindi cha kwanza kumalizika. 3. Singida walistahili penalty nyingine baada ya Che Malon kumvuta Sowah kwenye Box. 4. Singida walistahili penalty ya tatu baada ya Rupia kuchezewa vibaya na Hamza kwenye Box. Matukio makubwa manne yamezalisha matokeo ya 1-0 Singida kanyongwa mchana kweupe. Guys tuna miaka mingi sana mbeleni kumpata bingwa nje ya Kariakoo

Mukwala akamatiki

WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge, Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala dakika ya 43 akimalizia kazi nzuri ya kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua na kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 72, ingawa inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja tu na mabingwa, Yanga baada ya wote kucheza mechi 28.

Yanga yaibomoa ASEC Mimosas

Young Africans Spots Club kutoka Tanzania wanavutiwa na kocha Julien Chevalier raia wa Ufaransa Kwa sasa, Chevalier ni kocha wa ASEC Mimosas. Inasemekana mabingwa hao wa Tanzania bara wanataka kumchukua Mwalimu huyo Ili kuchukua nafasi ya Hamdi Miloud

Nabi aja kumaliza ishu ya Feitoto, sasa anaenda Kaizer Chiefs

Klabu ya Yanga SC awali waliweka million mia 800 ambazo walitaka kulipa Kwa awamu mbili ya kwanza mia 400 alafu wamalize 400 msimu mwingine , mwamba FEI TOTO akakataa akashinikiza pesa ilipwe yote Kwa pamoja. Klabu ya Simba wao fedha Yao waliweka mezani yote na mkataba kabisa wa FEI TOTO, Kiungo huyo hakuridhika na ofa ya Simba anaomba wajipange vizuri na warudi tena. Awali Klabu ya Kaizer chiefs walituma maomba ya kumwitaji Nyota huyo katika Klabu yake ya AzamFC lakini ofa Yao ilikuwa chini na AzamFC walitaka billion kadha ilikumwachia Kiungo huyo. Tarifa mpya Tena zinaripo kuwa tayari Kocha wa zamani wa Yanga ambae aliwahi kufanya kazi na Fei Salum Nabi ametua Tanzania kuzungumza na Kiungo huyo ili afanya nae kazi msimu ujao katika ligi kuu South Africa. Kuna vita Kubwa sana kuhusu uhamisho wa Kiungo FEI Salimu msimu huu na vita Kubwa inachezwa nje Yani viongozi wa Vilabu hivi vya Simba na Yanga yule mwenye kisu kikari Ndie atanufaika , tuendelee kusubiria

Jeuri ya pesa Yanga SC, Percy Tau ndani ya nyumba

Dau la kuvutia walilopata baada ya kuondoka kwa Stephane Aziz Kl Yanga, kumeifanya klabu hiyo mapema kuingia sokoni kumsaka mbaadala wake ambapo hadi sasa ina majina ya wachezaji wawili walio kwenye hatua nzuri ya kumalizana nao. Yanga SC imemuuza Aziz KI kwenda Wydad Casablanca ya Morocco na tayari nyota huyo ameondoka akiiacha timu hiyo ikimalizia Ligi Kuu Bara na fainali ya Kombe la FA. Katika kumpata mrithi sahihi wa Aziz KI, Yanga SC ipo kwenye mazungumzo na uongozi unaomsimamia winga wa zamani wa Al Ahly ya Misri, Percy Tau raia wa Afrika Kusini. Tau ambaye kwa sasa anaichezea Qatar SC aliyojiunga nayo Januari mwaka huu akitokea Ahly, inaelezwa hafurahishwi na maisha ya huko inapopatikana klabu hiyo yenye makazi yake jijini Doha. Uamuzi wa Yanga SC kuanza mazungumzo ya kumsajili Tau, ni uhitaji wao wa mchezaji ambaye atakuwa na uwezo mkubwa na kuisaidia timu kama ilivyokuwa kwa Aziz KI.

CR7 kuwavaa Real Madrid

Cristiano Ronaldo yuko na ofa mbili mezani kwa sasa moja ni kuongeza mkataba wa kubakia Al Nassr au Kukubali ofa ya Kujiunga na Al Hilal FC ili kupata nafasi ya Kucheza Kombe la Dunia la Vilabu Kama atakubali ofa ya Kujiunga na Al Hilal FC basi mchezo wake wa kwanza ni dhidi ya Real Madrid..

Simba kung' oa kiungo Fountain Gate

Baada ya kutoridhishwa na kiwango cha nyota Augustine Okejepha (21) inaelezwa Simba wameingia katika vita ya kuinasa saini ya nyota wa Fountain Gate Daniel Joram ambaye pia anawindwa na kikosi cha JKT Tanzania. Inaelezwa kocha Fadlu Davids alivutiwa na kiwango cha Joram hasa katika mchezo uliowakutanisha Simba na Fountain Gate na kumalizika kwa sare ya 1-1.

Simba yaihofia Singida Black Stars kesho

“Mechi ya Singida ni mechi ya kiporo na haiwezi kuwa rahisi, Singida ni moja ya timu ngumu sana, timu ambayo imewekeza, ina wachezaji wazuri, timu ambayo katika ligi inasumbua ila sisi kama Simba tumejipanga, pamoja na ugumu wao Singida lazima tupate matokeo ya alama tatu kesho” ''Suala la rotation lipo chini yetu waalimu, kwahiyo tutaangalia baada ya mazoezi ya leo, kikubwa ni kwamba timu nzima ipo kambini na wachezaji wote wapo vizuri, ni suala la benchi la ufundi kuona nani aanze na nani asianze. Fainali imeisha licha ya suala la saikolojia baada ya kupoteza mchezo wa fainali halikuwa sawa ila wachezaji wetu ni wakomavu baada ya fainali tulisema kwamba hili limekwisha, targate yetu sasa ni kuhakikisha tunapta kikombe Ligi kuu na hatuwezi kuwa mabingwa kama hatutoshinda mchezo wa kesho” - Seleman Matola Kocha Msaidizi Simba SC

Yanga yalamba milioni 945 kwa Wydad Casablanca mauzo ya Aziz Ki

Inaripotiwa kuwa Yanga SC wamepokea USD 350,000 (Tsh milioni 945) kutoka Wydad Casablanca kama sehemu ya kumnunua Azizi Ki aliyekuwa amesalia Mkataba wa mwaka mmoja Jangwani. Aziz Ki amepewa USD 150,000 (Tsh million 405) kama ada ya usajili kutokea Wydad na kusaini Mkataba wa miaka miwili. Wydad wamempa ofa ya mshahara mara mbili ya aliyokuwa anapewa Yanga na sasa analipwa USD 40,000 (Tsh milioni 107) kutoka USD 20,000 (Tsh milioni 53) aliyokuwa analipwa na Yanga SC. Kama ndivyo basi Stephano amezidi kukuwa toka ametoka Asec amekuwa akikua kiuchumi kila anaposaini Mkataba mpya.

Aziz Ki si sehemu ya kikosi Wydad kinachocheza na Sevilla

Kiungo Stephen Aziz Ki sio sehemu ya kikosi cha Wydad Casablanca ambacho kinacheza leo dhidi ya Sevilla ya Hispania. Mshambuliaji Mtanzania Selemani Mwalimu 'Gomez' yupo kwenye kikosi cha Wydad ambacho kinaivaa Sevilla leo usiku. Mechi hiyo ni sehemu ya maandalizi ya Wydad kwa ajili ya michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA 2025 inayotarajiwa kufanyika nchini Marekani kuanzia Juni 15 hadi Julai 13. Taarifa zaidi zinasema kwamba pamoja na mechi dhidi ya Sevilla ambao waliwasili jana Casablanca – Wydad pia watacheza na FC Porto ya Ureno Jumapili kukamilisha mbili za kirafiki kabla ya Klabu Bingwa ya Dunia.

Hersi aipongeza RS Berkane kwa kushinda ubingwa Afrika

Mwenyekiti wa Umoja wa Vilabu Afrika, Eng. Hersi Said anawapongeza sana Klabu ya RS Berkane kwa kubeba Ubingwa wa Kombe la Shirikisho la Afrika, siku ya jana Mei 25,2025, katika Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Berkane walibeba Ubingwa huo baada ya kuichapa Klabu ya Simba kwa jumla ya Mabao 3-1, Huku Klabu ya Simba ikiweka aibu ya ikipiga Shuti moja tu Lililolenga Lango [Shots On Target] ndani ya Dakika 180 za mechi za Fainali. Aidha, Eng Hersi amesisitiza kuwa, Pongezi zake kwa Timu Afrika atazitoa kwa mabingwa tu na si vinginevyo.

Manula kimeeleweka Yanga

Taarifa za kuaminika kutoka kwenye vyanzo vyetu vya habari kwamba mlinda mlango wa Simba SC Aishi Manula anaelekea kujiunga na watani zao Yanga SC kwenye dirisha kubwa lijalo. Manula ingawa anahusishwa kurejea Azam FC, lakini si kweli-, Yanga wameingia kwenye rada ya Manula na tayari kipa huyo amekubali kutua Yanga kufungana na swahiba zake Jonas Mkude na Clatous Chama. Manula atasaini mkataba wa miaka miwili, ingawa taarifa hazielezi mshahara wake na signing fee.

Simba kuadhibiwa na CAF

Kwa taarifa za awali ni kuwa Shirikisho la soka barani Afrika (CAF) lipo kufanya uchunguzi juu ya matukio mbalimbali kabla ya fainali mkondo wa kwanza na baada ya fainali ya mkondo wa pili ambapo kuna uwezekano mkubwa Simba ikakumbwa na rungu la Shirikisho hilo kutokana na mienendo ya Mashabiki wake lakini pia baadhi ya Viongozi Waandamizi wakumbana na adhabu kali, inatajwa hivyo kufuatia mtiririko wa matukio mbalimbali katika fainali hiyo. . Taarifa za awali zinadai pia kuna matamko na press mbalimbali za kulishutumu CAF kuhusiana na mabadiliko ya uwanja, hivyo wameanza rasmi kukusanya taarifa hizo ili kufanya maamuzi yake ikitajwa ni kuishutumu CAF na kutoa kauli za kichochezi dhidi ya Shirikisho hilo. .

Injinia Hersi awajibu Simba

Rais wa klabu ya Yanga, Injinia Hersi Said amewajibu wale walikuwa wakimshambulia mtandaoni kwamba kukaa kwake kimya si kuwaogopa isipokuwa anawavutiwa pumzi na sasa amewapa makavu. Wacha nieke hiki kitu wazi, kua kiongoz haimaanishi ukubali kejeli na matusi ya kila aina ya watu, kuna sehem unapaswa ukae kimya ila kuna mda uwape kile wanachokitaka. Wasichokijua wengi ni kwamba mm pia nmetokea maisha ya mtaani, nmeishi na wahuni, nmeishi uswahilini kwahyo ukija vibaya na unikute niko vibaya jibu utalipata. Kwa sababu wabongo mnahisi matusi ni dawa...ukija kweny page yngu na matusi usitegemee busara kwa sababu na mm ni binadam..mnalaumu sana sijafika uwanjani , hiv kitendo cha kuwafukuza mashabiki wa Yanga eti shughuli sio yao, sasa mimi shughuli ni yangu, hamjitambui.. #daimambelenyumamwiko, aliandika katika ukurasa wake

Azam Media yashinda kesi ya "Usiku wa vitasa"

Mahakama Kuu ya Tanzania imeipa ushindi Azam Media Limited katika kesi ya madai ya haki miliki iliyofunguliwa na bondia Amosi Mwamakula. Awali, Mahakama ya Kinondoni iliiamuru Azam Media Limited kumlipa bondia huyo kiasi cha shilingi milioni 250, baada ya kudai kuwa kampuni hiyo ilichukua wazo lake la kipindi cha “Boxing Kazi Kazi” kinachohusu masuala ya ndondi na kukitumia kwa jina la “Vitasa”. Hata hivyo, Mahakama Kuu baada ya kusikiliza shauri hilo imeipa ushindi Azam Media Limited kwa kuzingatia sheria za hati miliki. Wakili Neema Mbaga anayewakilisha Azam Media, amesema ushindi huo unaiwezesha Azam TV kuendelea na shughuli zake za kurusha vipindi vinavyohusiana na ndondi na mapambano mubashara ya ndondi.

Joshua Mutale arudishwa Chipolopolo

Kiungo Joshua Mutale amerejea kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Zambia baada ya kutokuwepo kwa kipindi kirefu. Mutale atakuwa sehemu ya kikosi cha timu ya taifa ya Zambia kitakachocheza mechi mbili za kirafiki za Kalenda ya FIFA dhidi ya Tunisia na Sudan.

Kaizer Chiefs yakaribia kumsajili Diarra

Klabu ya Kaizer Chiefs Inataka kutumia uhusiano wao mzuri na klabu ya Young Africans sc ili kumpata Djigui Diarra. Kaizer Chiefs wanatumia uhusiano huo kuwashawishi Young Africans ili wamuachie Djigui Diarra ili ajiunge kwenye klabu yao kwa dau watakalobkubaliana nao. Mpaka sasa bado Young Africans hawajajibu chochote juu ya mpango huo uliokaa kimtego huku pia Uongozi wa klab hiyo ukipitia ofa zaidi 5 zilizotumwa kwao juu ya kumpata mlinda lango huyo bora ndani ya ligi kuu ya NBC.

Mamelodi Sundown's yamrejesha straika wake wa Ethiopia

Klabu ya Mamelodi Sundowns Imrejesha Mshambuliaji wake Raia wa Ethiopia Aboubaker Nassir Ahmed aliyekuwa kwa mkopo katika klab ya SuperSport United. Aboubaker Nassir Ahmed ataungana na kikosi cha Mamelodi Sundowns kitakachoshiriki mashindano ya kombe la dunia kwa upande wa vilabu ( FIFA Club World Cup ) Mwezi ujao.

Yanga yaifanyia ubaya ubwela Simba

Taarifa nyepesi nyepesi Yanga SC ipo kwenye mchakato wa kufanya ubaya ubwela tena pale Simba SC, Baada ya goli kipa Camara kugombana na Ngoma, na hata vyumbani baada ya mechi Camara hakuonesha kuwa na ushirikiano na wenzake mzuri, Uongozi wa Yanga SC tayari umefanya mazungumzo na menejimenti ya mchezaji Camara jana usiku, Ili kuangalia uwezekano wa kumsajili goli kipa huyo ndani ya Yanga SC kuelekea msimu ujao, Yanga SC wanasubiria jibu kamili la menejimenti ya goli kipa Camara, Pia inaelezwa Camara ni shabiki mkubwa sana wa timu ya wananchi Yanga SC Hawa ndio Yanga SC, baada ya Chama Jr sasa ni zamu ya goli kipa Camara.

RSB Berkane yaiduwaza Simba New Amaan na kushinda ubingwa wa kombe la Shirikisho

NDOTO za Simba SC kutwaa Kombe la Shirikisho Afrika hazikutimia leo baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Renaissance Sportive de Berkane ya Morocco katika mchezo wa marudiano wa Fainali Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Matokeo hayo yanamaanisha RSB Berkane wanatwaa taji la CAF Confederation Cup kwa ushindi wa jumla wa 3-1 kufuatia kushinda mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita Uwanja wa Manispaa ya Berkane mjini Berkane. Katika mchezo wa leo Simba SC walitangulia kwa bao la Mzambia, Joshua Mutale Budo dakika ya 17 akimalizia pasi ya winga mwenzake, Mkongo Elie Mpanzu Kibisawala – kabla ya kiungo wa Kimataifa wa Mali, Soumaila Sidibe kuisawazishia RSB Berkane dakika ya 90’+3.

APR yatwaa ubingwa wa Ligi Kuu Rwanda mara 6 mfululizo

Klabu ya APR FC ya Jeshi nchini Rwanda imetwaa kombe la Ligi Kuu nchini humo baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Muhanzi United. APR FC imetwaa taji hilo wiki ya 29 ya Ligi Kuu ukiwa umesalia mchezo mmoja. Upande wa pili Rayon Sports walikuwa wenyeji wa Vision FC kwenye Uwanja wa Pele mjini Kigali bila Mashabiki ambapo walitoka sare ya 0-0 na kufikisha pointi 60 huku APR FC ikifikisha alama 64. Kwa ujumla ,APR FC imeshinda mataji 23 ya Ligi Kuu katika historia yake huku pia ikishinda taji la Amani 2025 na kurudisha rekodi ya kushinda Makombe mawili katika msimu mmoja baada ya kufanya hivyo mwaka wa 2014.

Ujenzi wa uwanja Simba waanza Bunju

Kampuni ya Jayruthy ambao ni wadhamini wa jezi wa klabu ya Simba SC, tayari wameanza utekelezaji wa ujenzi wa timu ya Simba maneno ya Bunju B jijini Dar es Salaam. "Suala la uwanja kwa Simba sasa sio stori tena, tayari tumempa Mkandarasi miaka mitano ambapo uwanja utajengwa pale MO Arena, Bunju na utekelezaji tayari umeanza huku tukitarajia kuwa na Mashabiki zaidi ya 20,000” Zubeda Sakuru, CEO wa Simba SC

Hamisa Mobetto hakuwa nyuma utambulisho wa Aziz Ki

Mwanamitindo maarufu nchini Hamisa Mobetto ambaye kwa sasa ni mke halali wa mchezaji Stephanie Aziz Ki hakuwa nyuma kwenye tukio la utambulisho wa mumewe ndani ya klabu ya Wydad Casablanca

Wydad Casablanca yamtambulisha Aziz Ki

KLABU ya Wydad Athletic imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki kuwa mchezaji mpya baada ya kukamilisha uhamisho wake kutoka Yanga ya Tanzania. Utambulisho huo umefanyika usiku wa kuamkia leo – saa chache tu baada ya Yanga kumuaga Aziz Ki kufuatia kuwa naye kwa misimu mitatu tangu awasili kutoka ASEC Mimosas. Wydad Athletic ya Morocco na usajili wake umeharakishwa ili akacheze michuano ya Klabu Bingwa ya Dunia ya FIFA inayotarajiwa kuanza Juni 14 hadi Julai 13 nchini Marekani ikishirikisha timu 32 kutoka Mabara sita – nne kutoka Afrika, nyingine ni Al Ahly ya Misri, EspĂ©rance ya Tunisia na Mamelodi Sundown ya Afrika Kusini.

Yanga yampa thank you Aziz Ki

Klabu ya Wydad Casablanca imethibitisha kumsajili kiungo mshambuliaji, Stephanie Aziz Ki kwa mkataba wa miaka miwili akitokea Young Africans ya Tanzania akiungana na wachezaji wengine waliosajiliwa na klabu hiyo kama Nordin Amrabat na Hamza Hanouri. Katika hatua nyingine Young Africans Sc imethibitisha kuwa nyota huyo raia wa Burkina Faso kuondoka klabuni hapo baada ya kutoa ‘Thank You’ kwa kinara huyo wa magoli kwenye Ligi Kuu bara msimu uliopita.

Rais Mwinyi kuwajaza mamilioni Simba wakitwaa ubingwa kombe la Shirikisho kesho

RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaahidi Simba SC dola za Kimarekani 100,000, zaidi ya Sh. Milioni 250 iwapo watatwaa Kombe la Shirikisho Afrika kesho. Simba SC watamenyana na RSB Berkane ya Morocco kesho kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar wakihitaji kupindua matokeo ya kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita nchini Morocco ili watwae taji hilo. Na jioni ya leo Rais Mwinyi amewatembelea Simba SC kambini kwao na kuzungumza na wachezaji na makocha pamoja na viongozi kuwapa motisha kuelekea Fainali hiyo ya kihistoria kesho.