RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi amewaahidi Simba SC dola za Kimarekani 100,000, zaidi ya Sh. Milioni 250 iwapo watatwaa Kombe la Shirikisho Afrika kesho.
Simba SC watamenyana na RSB Berkane ya Morocco kesho kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar wakihitaji kupindua matokeo ya kufungwa 2-0 kwenye mchezo wa kwanza Jumamosi iliyopita nchini Morocco ili watwae taji hilo.
Na jioni ya leo Rais Mwinyi amewatembelea Simba SC kambini kwao na kuzungumza na wachezaji na makocha pamoja na viongozi kuwapa motisha kuelekea Fainali hiyo ya kihistoria kesho.