Shirikisho la mpira wa miguu duniani FIFA limepitisha maazimio mapya 3 yanayohusu masuala ya ubaguzi kwenye mpira wa miguu.
Maazimio hayo ni kama yafuatayo:
- Mchezaji ambae atafanyiwa ubaguzi wa aina yoyote kama vile, ubaguzi wa rangi,ubaguzi wa kiraia,jinsia n.k atatakiwa kumpa taarifa mwamuzi wa mchezo husika,Kisha mwamuzi huyo atasimamisha Mchezo huo au kusitisha moja kwa moja na timu zote kuondolewa kwenye pitch.
- Klabu ambayo mashabiki wake, Viongozi wake, wachezaji wake,kama watakuwa wamehusika kwenye tukio lolote la ubaguzi kwa mara ya kwanza kuanzia maazimio haya yaanze kufanya kazi,watatozwa faini yenye kiasi Cha $6M.
- Endapo klabu yoyote itarudia zaidi ya mara moja kuhusika kwenye kesi za ubaguzi wa aina yoyote Ile klabu hiyo,itakumbana na adhabu moja kati ya hizi 3 au zote Kwa pamoja:
*Kuzuiwa kuingiza mashabiki kwenye mechi za nyumbani zote zilizosalia.
*kukatwa alama kutoka kwenye msimamo wa mashindano husika.
*Kufutiwa leseni ya kushiriki kwenye mashindano husika,pamoja na kushushwa daraja moja kutoka walilopo.