Ujio wa kocha Nasredine Nabi ndani ya Tanzania hauhusiani chochote na sakata la Usajili wa mchezaji Feisal Salum, kama nilivyoeleza majuma kadhaa nyuma.
Hakuna mawasiliano ya moja kwa moja baina ya Kaizer Chiefs na Azam FC juu ya usajili wa Feitoto, Nabi hahusiki na usajili wa Kaizer Chiefs akishapendekeza jina la mchezaji kazi inafanywa na uongozi wa klabu.
Feisal ana mkataba na Azam Fc, na mpaka sasa timu inayoonekana iko serious na deal ya Feisal ni Yanga nyengine zinabaki kuwa tetesi tu.