Baada ya msanii Matilda au Matty kutoonekana kwenye series ya Dunia, na kuzua sintofahamu huku wengi wakidai kwamba msanii huyo anaumwa na amelazwa.
Mambo Uwanjani Blog inawajuza wadau wake kwamba taarifa iliyowahi kutolewa na blogu hii kwamba Matilda hatoonekana kwenye series hiyo ni za kweli na sasa hayupo kwenye Dunia.
Msanii huyo hata kama anaumwa au aumwi, lakini kilichomuondoa kwenye series hiyo ni kwamba mume anayetaka kumuoa ama mchumba wake hataki kuona mkewe au mchumba wake akiendelea na sanaa.
Wadau wa Dunia wanatakiwa kuwa wavumilivu na wakubali matokeo kwamba Matilda au Matty si msanii Tena kwenye series hiyo maarufu kwasasa.