IVO Philip Mapunda ni miongoni mwa makipa bora katika historia ya soka la Tanzania, akijulikana kwa umahiri wake wa kupangua penalti na kudhibiti mashambulizi hatari. Alizaliwa Novemba 14, 1979, katika kijiji cha Kisa Ushirika, Safari yake ya soka ilianzia katika viunga vya Kisa Ushirika, Tukuyu Mbeya, mji wenye mandhari nzuri ya milima, mashamba ya chai, na hali ya hewa ya baridi, kisha kusambaa hadi nje ya mipaka ya Tanzania, akitamba katika vilabu kadhaa Akiwa mdogo, alisomea Kisa na Nyololo, kisha akasoma Mechanics katika Shule ya Ufundi Ifunda. Ingawa alipata nafasi ya kuendelea na masomo ya ufundi, aliamua kufuata ndoto yake ya soka. Alianza kucheza Mpuguso Stars kisha Tukuyu Stars, ambapo aling’arisha kipaji chake kabla ya kusajiliwa na Tanzania Prisons. Akiwa Prisons, aliingia rasmi Jeshi la Magereza na kuwa Koplo, lakini alipotaka kuihama timu, alikumbwa na matatizo hadi kufungwa jela. Baada ya kutoka, alijiunga na Moro United (2005), kisha akasajiliwa na Yanga SC (2006-2009)....