Shirikisho la soka Afrika (CAF) limetangaza orodha ya Waamuzi watakaoshiriki katika mafunzo yatakayofanyika kuanzia tarehe 11 hadi 15 Machi 2025 mjini Abidjan, Ivory Coast kwa ajili ya kujiandaa na Michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika na Kombe la Shirikisho Afrika.
Ndabihawenimana ni miongoni mwamuzi wa kimataifa wa Burundi mwenye umri wa miaka 39 (aliyezaliwa 5 Machi 1985) ambaye amewekwa katika orodha hiyo huku Tanzania ikikosa hata mmoja.
Mafunzo hayo yatahusu matumizi ya teknolojia ya kisasa ya VAR ambayo itatumika katika hatua ya robo fainali ya michuano ya Afrika.
Pacifique Ndabihawenimana amejulikana katika mashindano ya kufuzu kwa kombe la mataifa ya Afrika na mashindano makubwa ya Afrika kama vile ligi ya mabingwa wa CAF na kombe la shirikisho CAF.