Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Januari, 2025

Tumezoea kutoa bonus kwa wachezaji wetu- Mwagala

Msemaji wa Tabora United Christina Mwagala amemshangaa Afisa Habari wa Simba SC, Ahmed Ally kuhusu wachezaji wa Tabora United kupewa bonus ya shilingi milioni 50 endapo wataifunga Simba Jpili. "Mie namshangaa sana Ahmed anakuwa muoga muoga, mtoto wa kiume hutakiwi kuwa muoga nilazima ukabiliane na tatizo ambalo utakutana nalo. Inshu ya Bonus ndio naona watu wanaikuza kuza ila sisi bonus tumeanza kupewa tangu tumeanza Msimu na mkuu wetu wa Mkoa, Timu ikitoa sare ni milioni 5, ikishinda ni milioni 10. Lakini kuelekea mchezo dhidi ya Simba amewiwa kutuongezea dau la milioni 50, kwahiyo imekuwa kawaida yetu kula na kunywa na mkuu wetu wa Mkoa wa Tabora.'' Christina Mwagala, Afisa habari wa Club ya Tabora United.

Aziz Ki awaaga Wanayanga

Mfungaji Bora wa msimu uliopita wa Ligi Kuu bara ya NBC Primier League na timu ya Yanga SC Stephanie Aziz Ki ameanza kuwaaga mashabiki wa timu hiyo na akidai kwamba hatoendelea kusalia kwenye ardhi ya Tanzania. Uongozi wa Yanga chini ya Rais wake Injinia Hersi Said alitangaza kuwauza Aziz Ki na Clement Mzize na kwa mujibu wa taarifa tulizozipata kwamba nyota hao wawili wameuzwa. Aziz Ki na Mzize inasemekana watajiunga na Klabu ya Al Itrihad ya Libya na ikiwapa Yanga mabilioni ya shilingi. Aziz Ki anatumia muda huo kuwaaga mashabiki wa Yanga ambao amekaa nao vizuri na kuweza kuwaletea mafanikio kadhaa na yeye akishinda tuzo ya mfungaji Bora na mchezaji Bora (MVP) wa Ligi hiyo

Morrison kuikosa Yanga Februari 5

Winga mpya wa klabu ya KenGold FC, Bernard Morrison ataikosa michezo ya awali ya mzunguko wa pili wa Ligi Kuu bara ya NBC kutokana na kuwa hajakuwa sawa kucheza uwanjani kutokana na jeraha ambalo alikuwa anajiuguza. Bernard Morrison alifanyiwa upasuaji wa goti ambao ulimfanya akae nje msimu mzima. Bernard Morrison ataukosa mchezo kati ya KenGold FC dhidi ya Yanga SC utakaopigwa Februari 05, katika uwanja wa KMC Complex. Morrison kwasasa anafanya mazoezi maalumu ya pekeake bado hajaanza kufanya mazoezi na wachezaji wenzake.

Seleman Mwalimu atambulishwa Wydad Casablanca

Klabu ya Wydad Casablanca imekamilisha Usajili wa Nyota wa Klabu ya Singida Black Stars anayecheza kwa Mkopo Seleman Mwalimu . Ikumbukwe Wydad walikua wanamuhitaji Clement Mzize katika dirisha hili la Usajili lakini Yanga wamewapiga Kalenda hadi mwezi Julai mwaka huu. Mwalimu pia alikuwa anaichezea Fountain Gate lakini Singida Black Stars walimnunua na sasa wamempiga bei

Ahmed Ally atoa sababu kutoitwa na CAF

Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ametoa ufafanuzi kuhusu kutokuwepo kwake kwenye hafla ya upangaji wa makundi ya AFCON 2025 inayotarajiwa kufanyika Januari 27 nchini Morocco. Akizungumza kupitia vyombo vya habari, Ahmed Ally alisema: "Mimi CAF hawawezi kunifuata kwa sababu nina ratiba ya kuandaa timu kuelekea Robo Fainali, kwahiyo CAF wanaangalia nani hana kazi, ndiyo maana wanamualika yaani Jobless." Kauli hii ilikuja baada ya taarifa kwamba Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe, amepata mwaliko wa kuhudhuria hafla hiyo kutoka Shirikisho la soka la Afrika, CAF. Ahmed Ally alisisitiza kuwa majukumu yake ndani ya Simba SC ni muhimu zaidi kwa wakati huu, hasa katika maandalizi ya timu kuelekea hatua ya Robo Fainali ya michuano inayoendelea

Aslay kutua WCB, Mbosso nje

Baada ya msanii Babalevo kutangaza kuwa Mbosso_ yuko mbioni kuondoka katika Label ya WCB WASAFI, pia alitangaza ujio wa wasanii wapya tisa ( 9 ) ambao wanaweza kujiunga na Label hiyo mwaka huu. Ikumbukwe pia C E O wa Label hiyo Diamond Platnumz amekuwa akilitaja jina la msanii Aslay mara kwa mara kumpa maua yake kwa uwandishi wake mzuri na kipaji chake kwa ujumla. "Aslay ni msanii mzuri sana ila anakwamishwa na uongozi wake kama Aslay angekuwaga WCB angefikaga mbali sana " hayo ni baadhi ya maneno aliyowahi kuzungumza Diamond Platumz huko nyuma. Leo Januari 31 msanii Baba Levo amechapisha (post) picha ya msanii Aslay na kuweka alama za shukrani. Swali ni Je Aslay amekubali kuichukua nafasi ya Mbosso WCB na vipi Aslay anaweza kuliziba pengo la Mbosso WCB WASAFI ? Mbosso

Yanga yatajwa kuongoza kwa mashabiki wengi Tanzania

Kwa mujibu wa Africa Facts Zone Timu ya Yanga ina jumla ya wafuasi milioni 35 kote duniani huku timu ya Simba wakiwa na wafuasi milioni 10 tu pitia Orodha hii taratibu Al Ahly 🇪🇬 - 70 million Young Africans SC 🇹🇿 - 35 million Zamalek 🇪🇬 - 30 million Kaizer Chiefs 🇿🇦 - 16 million ASEC Mimosas 🇨🇮 - 15 million Manchester United 🇬🇧 - 1.1 billion Arsenal 🇬🇧 - 630 million Chelsea 🇬🇧 - 509 million Liverpool 🇬🇧 - 500 million Milan 🇮🇹 - 500 million Inter 🇮🇹 - 500 million Juventus 🇮🇹 - 440 million Real Madrid 🇪🇸 - 400 million Barcelona 🇪🇸 - 300 million Flamengo 🇧🇷 - 50 million Corinthians 🇧🇷 - 30 million Galatasaray 🇹🇷 - 30 million Fenerbahce 🇹🇷 - 25 million River Plate 🇦🇷 - 20 million Palmeiras 🇧🇷 - 21 million Boca Juniors 🇦🇷 - 16 million Atletico Nacional 🇨🇴 - 15 million Santos 🇧🇷 - 13 million ASEC Mimosas 🇨🇮 - 15 million fans Asante Kotoko 🇬🇭 - 10 million fans Celtic 🏴󠁧󠁢󠁳󠁣󠁴󠁿 - 10 million fans Simba SC 🇹🇿 - 10 million fans Raja Casabla...

Tshabalala amkaribisha Chama Msimbazi

Baada ya kiungo mshambuliaji Clatous Chama ambaye kwasasa anaichezea Yanga kudai kwamba atarejea Simba kumalizia soka lake (kustaafu). Mchezaji mwenzake Mohamed Hussein Tshabalala amemjibu na kumkaribisha Msimbazi lakini wenye timu yao watakapoamua. Chama aliichezea Simba kwa mafanikio na msimu amejiunga na Yanga lakini hajawa na furaha kutokana na kuwekwa benchi na makocha wote wawili (Gamondi) na (Ramovic) hivyo anatamani kurudi Msimbazi. "Nimeona hii taarifa kaka kua unahitaji kuja kuitumikia Simba na kustaafu ukiwa Simba sio wazo baya ni wazo zuri ila wenye Simba ni mashabiki wao ndio watatoa maamuzi sahihi", alisema Tshabalala beki wa kushoto wa Simba SC

Yanga wamepata tiba fasta

BAADA tu ya kutolewa katika Ligi ya Mabingwa Afrika, vigogo wa Yanga waliitana haraka na kufanya tathmini ya kile ambacho kimewakwamisha na kupitia kikao hicho yapo waliyoyabaini na kuna maamuzi walichukua, ikiwamo kuigusa kamati ya mashindano ya klabu hiyo. Kwanza kwa pamoja walikubaliana kwamba timu yao ilistahili kupata ushindi dhidi ya MC Alger ya Algeria katika mechi ya mwisho ya makundi katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, wikiendi iliyopita ambayo iliwakwamisha kumaliza nafasi ya pili kwa Kundi A na kuvuka kwenda robo fainali. Pili waligundua utaratibu wa wachezaji kufanya mazoezi wakitokea nyumbani na kisha kukutana siku chache kabla ya mechi unawapa uhuru uliopitiliza ambao unaleta athari hasi kwa timu. Kutokana na hilo, klabu hiyo imepanga kufanya mambo mawili ambayo inaamini yatakuwa suluhisho kwa siku za usoni. Jambo la kwanza ambalo imeamua kulifanya ni kufanya maboresho ya kamati ya mashindano na kuna baadhi ya watu itawapunguza na wengine kuongezwa ili kuipa nguvu zaidi. ...

Sikutamani kuichezea Yanga - Sureboy

Salum Abubakar ( Sure Boy) miongoni mwa mahojiano yake aliyowahi kufanya na AzamTV Alisema hivi “ Mimi ni mshabiki wa yanga toka nikiwa mtoto nimekua katika familia ambayo wanapenda yanga kwahiyo hata Mimi nilikuwa napenda Yanga , sikutamani kucheza Yanga hapa awali kwasababu nilikuwa najua nitaumia alafu mashabiki wataumia sana , Yanga timu yenye mashabiki wengi ambao wanapenda sana timu yao ”, Kwanini nimeandika nukuu hii ? Vijana wengi wanaocheza soka wanandoto za kucheza Simba na Yanga lakini hawajui njia nzuri ya wao kufika hapo, fikiria kama sure boy angetaka kwenye yanga toka muda kipindi kile umri na energy ni nyingi ingekuwaje angeshindwa ? Vijana katika soka waambie wawe na uvumilivu na sehemu walizopo mafanikio katika soka hayataki haraka. mara kadha ambazo sure boy anapata nafasi katika Kikosi cha Yanga kwasasa bado Kiwango chake kinatoa majibu kwa vijana kuwa unatakiwa kuheshimu mpira na kuishi katika misingi ya soka. 1 : Utulivu mkubwa Mali inapokuwa mguuni 2 : Pasi eleke...

Chama aiota Simba

Kiungo mshambuliaji wa kimataifa wa Zambia anayechezea Yanga iliyoondolewa hatua ya Makundi Ligi ya Mabingwa Afrika Clatous Chama amefichua kuwa pindi atakapokuwa anaelekea kustaafu soka ndoto zake ni kurudi kuichezea Simba kwa mara nyingine. “Nikikaribia kustaafu, timu ya kwanza kuipa kipaumbele cha kuichezea ni Simba ila kama wakinikataa ndio ninaweza kwenda timu nyingine kumalizia soka,” alisema Chama.

Tshabalala amuanika Layka

Baada ya jana mshambuliaji hatari wa mabingwa wa soka Tanzania bara Prince Dube kupost picha akiwa na watoto wake. Beki wa kushoto wa vinara wa Ligi Kuu bara Mohamed Hussein Tshabalala au Zimbwe Jr naye amepost picha akiwa na mwanaye aliyemtambulisha kwa jina la Layka. Tshabalala ameenda mbali zaidi kwa kusema mtoto wake Layka anaonekana ni Simba damu.

Goztepe ya Uturuki yamuulizia Mzize

Beki wa kushoto wa Klabu ya Goztepe ya Uturuki Novatus Dismas raia wa Tanzania amesema kwamba Clement Mzize ni mmoja kati ya mchezaji aliyekuwa akitajwatajwa na viongozi wake yake. "Zaidi ya mara mbili viongozi wangu waliniulizia Mzize na hasa baada ya mechi ya Yanga na TP Mazembe baada ya kuona video zake naamini ni suala la kusubiri." Amesema Novatus Dismas NBeki wa kushoto wa Göztepe ya Uturuki Novatus Dismas

Msuva atupia tena Iraq

Nyota wa Tanzania Simon Msuva ameisaidia timu yake ya Al Talaba kupata ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Iraq dhidi ya Karbalaa FC. Msuva amefunga bao moja kwenye mchezo huo.

KUTOA URAIA KWA WACHEZAJI WA KIGENI SIO SAHIHI

Na Abdul Makambo SUALA la kutoa uraia kwa wachezaji wa kigeni silipingi ila linatia shaka.lazima tulitazame kwa jicho pana vinginevyo tutafeli. Hawa wachezaji wengi hawana ubora katika nchi zao ndiyo maana wamekuja katika ukanda wetu wa CECAFA. Tuachane na mtizamo huo tunachotakiwa tutengeneze program ya kuibua vipaji vya soka. Tanzania imebarikiwa kuwa na vipaji vya soka.tukijipanga tunaweza hata Roma haikujengwa siku moja na penye nia pana njia.

Zungu wa Wasafi Media awaaga na kuwashukuru

Mtangazaji wa vipindi mbalimbali wa redio Wasafi, Zungu ameishukuru redio kwa kumlea vema na kumtangaza. Wasafi Media mna zawadi yenu kubwa mbinguni, tangu nilipoanza kazi hapo mwaka 2020 hakika chini yenu nimetumika na kukua vyema, nimepata connection nyingi kwa msaada wenu nyinyi ni watu wema sana mlinitambulisha zaidi duniani na kunishika mkono! Lipi kubwa zaidi ya asante kwenu Wasafi Media, sasa hesabu zinaniambia umefika wakati wa kwenda kukua zaidi na kutumika sehemu nyingine, kwenda kutafuta changamoto nyingine na kuitumia zawadi hii aliyonibariki Mungu sehemu nyingine.

Uraia pacha umeshindikana, kubadili uraia inawezekana

Na Prince Hoza VYOMBO vya Habari hapa nchini vilikuwa vinapiga kelele kila kukicha suala la kutaka nchi iruhusu uraia pacha ili iwe rahisi kwa nchi yetu kufaidika na wanamichezo wetu wanaoishi ughaibuni kuzisaidia timu zetu za taifa. Vilio vilikuwa vikubwa kiasi kwamba kuliomba bunge letu tukufu la Jamhuri ya muungano wa Tanzania ili kuweza kubadili vifungu vya Sheria kwenye katiba yetu iliyopo. Lakini licha ya kuomba sana, bunge letu tukufu likashindwa kuridhia maombi hayo huku baadhi ya wabunge wakakataa maombi hayo wakidai sababu za kiusalama. Watanzania waliona nchi kama inachelewa katika upande wa michezo, kwani kila msimu timu zetu za taifa zinatolewa mapema katika michuano mbalimbali inayoshiriki. Timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ni miongoni mwa timu zilizowaliza wengi baada ya kushindwa kwake kufuzu katika michuano iliyokuwa inashiriki, kwa mfano Stars ilishindwa kufuzu michuano ya mataifa Afrika, AFCON na kombe la Dunia. Kushindwa kwake kufuzu, kuliwafanya wadau wa soka ...

Prince Dube akiwa na watoto zake nyumbani

Mshambuliaji hatari wa mabingwa wa soka Tanzania bara, Prince Dube Mpumalelo, amepost picha yake akiwa na watoto wake wawili. Katika picha hiyo Dube anaonekana kuwa na furaha, inaonekana wazi kwamba Dube ana watoto wawili wadogo wanaolingana.

Chippa United yamtema Majogoro

Kiungo wa timu ya taifa ya Tanzania Baraka Majogoro ameachana na klabu yake ya Chippa United kwa makubaliano ya pande zote mbili. Majogoro (27) ambaye alijiunga na miamba hiyo ya Afrika Kusini mnamo Agosti 2023 akitokea KMC Majogoro amekosa mechi tano tu kwenye michuano yote klabuni hapo msimu huu. Nyota huyo wa zamani Ndanda Fc, Polisi Tanzania na Mtibwa Sugar kwa sasa ni mchezaji huru na upo uwezekano wa kuendelea kukipiga Afrika Kusini huku vilabu kadhaa vikitajwa kuhitaji saini yake.

Nyota wa Tanzania ang' ara Mexico

Nyota wa Tanzania Julitha Singano akiwa na timu yake ya FC Juarez wameibuka na ushindi wa mabao 2 -1 dhidi ya Santos Laguna kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Mexico uliochezwa wikiendi

Maxi Nzengeli awatoa presha Wanayanga, afikiria mechi ya Kagera Sugar Jmosi

"Mimi sihusiki na tetesi,tetesi ni zenu nyie ili muuze habari. Mimi nafanya kazi yangu kama mwajiriwa wa Yanga. Kama niko hapa Yanga kwa mkopo mimi silijui hilo na wala sitaki kujua nilinunuliwa pia sijui. Lakini na nyie muwe mnajihoji Mwenzangu Mayele walisema hivyohivyo kuwa yupo kwa Mkopo lakini alicheza miaka 2 na kuuzwa na Yanga kwenda Pyramid. Kitu kikubwa ninachokiwaza je kocha atanipa nafasi Jumamosi niweze kuitetea nembo ya mwajiri wangu Yanga? Niulize hilo swali. Maxi Nzengeli mchezaji wa Yanga anayemezewa mate na Timu kibao Tanzania na Afrika Kusini.

Bernard Morrison afurahia kutua KenGold

Benard Morrison, maarufu kama BM3, ameelezea furaha yake kwa kujiunga na Kengold FC huko Chunya, Mbeya, wakati wa mahojiano ya kipekee na Radio Dream FM.  Akizungumzia safari yake ya mafanikio akiwa na klabu kubwa za Tanzania, Simba SC na Yanga SC, Morrison anasema uhamisho wake kwenda Kengold ni hatua mpya iliyojaa malengo na fursa. Anasifu maono na ari ya klabu hiyo. Akisisitiza kujitolea kwake kuleta uzoefu, uongozi, na mtazamo wa ushindi kwa timu. Morrison pia anaonyesha hamu yake ya kuhamasisha wachezaji wachanga na kusaidia klabu kufanikisha mafanikio makubwa, akiahidi mashabiki na wafuasi wake kujituma kwa hali na mali.

Tabora United wakamilisha vibali vya wachezaji wake wa kigeni, Simba sasa kazi wanayo

Hatimaye Tabora United wamefanikiwa kulipia vibali vya Wachezaji wote saba waliosajiliwa dirisha dogo. Mwanengo, Mustapha, Akandwanaho, Cedric Zemba, Fikirini, Jean Noel na Chobwedo Wamekamilishiwa taratibu za kupata leseni.

Mwamuzi wa Tabora United na Simba SC huyu hapa

Amina Kyando ndiye mwamuzi atakayechezesha mechi ya Ligi Kuu ya NBC kati ya Tabora dhidi ya Simba Feb. 2 ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi Mbali ya Kyando kusimama katikati, wasaidizi ni Luhemeja na Fatma Mambo Mara ya mwisho kwa Amina kuchezesha mechi ya timu hizi ni Mei 6, 2024 Simba ikishinda 2-0

Eliza Tungu mwamuzi chipukizi wa soka

Anaitwa Eliza Tungu ni mshika kibendera anaetumika zaidi kwenye michezo ya ligi za vijana pamoja na Ligi ya wanawake nchini Tanzania. Bado yupo katika hatua za awali kabla ya kupandishwa hadhi na kuwa miongoni mwa waamuzi wasaidizi watakaotumika kwenye michezo ya Ligi Kuu bara pamoja na michezo ya kimataifa iliyopo chini ya CAF na FIFA. PISI MOJA KALI SANA 🔥🙌🥰

Yanga kubomoka, Aucho naye agoma kusaini

Kiungo wa kimataifa wa Uganda Halid Aucho amemwambia kocha wa klabu hiyo kuwa hataongeza mkataba mpya. Hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote baina ya Yanga na Aucho licha ya kwamba mkataba wake unatamatika mwezi juni mwaka huu. Pia, kuna taarifa zinazoeleza kuwa nyota huyo ametumiwa ofa ya kwenda kukipiga kunako ligi ya Saudia

Msimu ujao rukhsa kucheza timu mbili CAF

Kuanzia Msimu ujao, mchezaji atakayesajiliwa Dirisha Dogo ataruhusiwa kucheza Michuano ya CAF katika Timu yake mpya hata kama mchezaji huyo alishacheza michuano hiyo kwenye Timu aliyotoka. Hii ni kwa Mujibu wa Mabadiliko mapya ya kanuni zilizopitishwa na chama cha Vilabu kupitia Mwenyekiti wake Hersi Said Ally.

Kaizer Chief kumng' oa Tshabalala Simba

Kocha Mkuu wa klabu ya Kaizer Chiefs Nasreddine Nabi, imedaiwa kuwa anatafuta Beki wa kushoto na tayari amelipendekeza jina la Beki wa klabu ya Simba Mohamed Hussein kwenye uongozi wa klabu hiyo. Nabi amewasisitiza mabosi wa klabu hiyo kuwa atafurahi kama ataletewa Tshabalala kutokana na ukweli anaujua uwezo wake, Kwani Lengo lake ni kuona upande wa kushoto wa ukuta wa Timu hiyo unaimarishwa zaidi. Mkataba wa Tshabalala na Simba utamalizika mwishoni mwa msimu huu na Kaizer inapiga hesabu kama itamkosa kwa sasa basi itasubiri beki huyo hadi mwisho wa msimu ili impate kiulaini. Katika msimu huu beki huyo amecheza mechi zote za kimataifa na kufunga bao moja, huku katika Ligi Kuu Bara akifunga bao moja na kuasisti mara tatu.

CAF, TOTALENERGIES WAONGEZA MKATABA

Shirikisho la Soka Barani Afrika CAF pamoja na TotalEnergie wanaongeza Mkataba mpya wa udhamini. Tukio hilo litafanyika January 28, siku ya jumanne katika Hotel ya Hyatt Regency Jijini Dar es Salaam. Watakuwepo Rais wa CAF Patrice Motsepe, Mwenyekiti na CEO wa TotalEnergies Mr Patrick Pouyannè.

Yanga yampotezea Musonda

Uongozi wa Klabu ya Yanga haupo kwenye mazungumzo yeyote ya kuongeza mkataba mpya na Mshambuliaji wao raia wa Zambia Kennedy Musonda (29) ambaye walimsajili Msimu wa 2022/23 akitokea Power Dynamos ya nchini Zambia Musonda kwa sasa anapitia kipindi kigumu ndani ya kikosi cha Yangu . Kipindi ambacho kinamwandama musonda kimeambatana na kuporomoka kwa kiwango chake ndani ya kikosi cha Yanga Vilabu vya Tp Mazembe, Al ittihad Qatar, vimeonyesha nia ya kumhitaji nyota huyo pindi tu dirisha kubwa litakapo funguliwa na kama hatoongeza mkataba na Yanga

1998 Yanga waliazima jezi za Taifa Stars

Mwaka 1998 Yanga walicheza hatua ya robo fainali ya CACL kwa mara ya kwanza dhidi ya Asec Mimosa ya Ivory Coast. Lakini cha kuvutia zaidi katika mchezo huo ni Yanga walipoazimwa jezi za timu ya taifa (Taifa stars) ili wazitumie katika mchezo huo,lakini pia waliazima wachezaji kutoka Simba ili wawasaidie na pamoja na msada huo bado Yanga alifungw bao 3 kwa 0 katika dimba la uhuru. Wachezaji walioazimwa toka Simba ni Monja liseki na Shaaban Ramadhani. Yanga waliazima jezi za Stars sababu walikua na jezi za njano tu ambazo zilifanana rangi na jezi za Asec.

Rio Ferdinand amjia juu kocha Man U

Beki wa zamani wa Manchester United, Rio Ferdinand anaamini, Marcus Rashford (27) hana mustakabali tena katika klabu hiyo baada ya meneja, Ruben Amorim kusema afadhali kuwa na kocha wake wa makipa katika kikosi chake kuliko kuwa na Rashford. Rashford hajaichezea United tangu Desemba 12, huku Amorim akimuacha nje ya kikosi kwa kila mechi kando na mchezo mmoja, ambao alikuwa akitokea benchi na hakutumika. Alipoulizwa kwa nini hakumjumuisha Rashford katika mechi ya Jumapili ya 1-0 dhidi ya Fulham, Amorim alijibu ni bora kumchezesha Kocha wa Makipa Jorge Vital, mwenye umri wa miaka 63. “Sote tuna siku za mbaya au wakati ambapo hatufanyi vizuri, tunakosa kujiamini, lakini bidii sio moja ya mambo ambayo ningetaka kusikia kutoka kwa meneja akisema kuwa ni chanzo cha mimi kupungukiwa. “Hayo ni maoni ya kuchukiza, kwa sababu nadhani anajua majibu ni nini baada ya maoni hayo. Hasemi hivyo bila kufikiria, ‘Hii inaelekea wapi?’ Kwa kweli hakuna njia ya kurudi kwa Marcus baada ya hapo, sidhani, na ...

Yanga sasa kumuuza Mzize

Baada ya kupokea ofa nyingi kutoka klabu mbalimbali, klabu ya Yanga imelegeza msimamo na sasa huenda ikamuuza mshambuliaji Clement Mzize katika dirisha lijalo la usajili, imefahamika Wakati klabu nne za Uarabuni zikisubiri majibu ya Yanga juu ya utayari wao wakiwa tayari wameshaweka fedha ndefu mezani, taarifa mpya ni kwamba kuna klabu nyingine ya Ulaya nayo imepiga hodi ikimtaka mshambuliaji huyo. Ukiacha ofa za klabu hizo kutoka Afrika Kaskazini zinazofikia Sh2 Bilioni, klabu hiyo ya Ubelgiji inataka kutoa zaidi ya fedha hizo kufikia 2.5 bilioni. Mmoja wa maafisa waandamizi wa Yanga amedokeza uwezekano wa Mzize kuuzwa baada ya klabu kuvutiwa dau hilo lakini muhimu zaidi ni kuzingatia maslahi ya mchezaji “Tunafikiria kufanya biashara fedha zinazosemwa ni nyingi unajua pia tunataka kufikiria juu ya maisha ya baadaye ya mchezaji ili akajiendeleze tutaangalia ofa ipi itakuwa sahihi zaidi kwa klabu na kwake,” Afisa huyo alinukuliwa na Mwanaspoti Msimu huu Mzize yuko ‘on-fire’ akifunga mab...

Mmiliki Alliance afariki dunia

Aliyewahi kuwa Meya wa Jiji la Mwanza ambaye pia ni Mmiliki wa Shule za Alliance (Alliance Schools), James Marwa Bwire amefariki Dunia usiku wa Januari 25 akiwa jijini Mwanza baada ya kuugua kwa muda mrefu. Ukurasa rasmi wa Instagram wa klabu ya Alliance Football Club umethibitisha kifo cha Bwire ambaye ni muasisi wa Alliance School Sports Academy, ambayo inamiliki timu mbili za Alliance Girls inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake (WPL) na Alliance Football Club inayoshiriki First League. Alliance Academy imeibua vipaji vya wacheza soka wengi wa kiume na wa kike kama Aisha Masaka anayekipiga katika Ligi Kuu ya Wanawake England akiwa na timu ya Brighton. Aisha Mnunka anayekipiga Simba Queens, Israel Patrick Mwenda anayekipiga Yanga, Hance Masoud Msonga ambaye yupo KMC na wengine wengi. Mmiliki wa Alliance James Bwire (kulia) amefariki

Nabi bado anamtaka Mayele

Fiston Mayele bado yupo kwenye Rada za klabu ya Kaizer Chiefs.. Klabu Mpya kutoka Nchini Saudia Arabia waliwasilisha ofa yao rasmi . Al Riyadh Football imetoa zaidi ya euro milioni 1 kumkaribisha mfungaji huyo wa Kongo, mazungumzo yanaendele na klabu yake ya Pyramid FC ya nchini Misri.

Ibrahim Class apanda ubora

BONDIA wa ngumi za kulipwa Ibrahim Class amepanda katika ubora baada ya kufikisha nyota nne kutoka tatu na nusu aliyokuwa nayo kwa muda mrefu. - Class aliweka taarifa hizo kwenye mtandao wake na kusema kuwa Mwenyezi Mungu, bidii, sapoti ya familia, mashabiki na timu yake vimemuwezesha kufikia hatua hiyo. - “Hii ni heshima kubwa na motisha ya kuendelea kupambana zaidi bila kuchoka,”amesema na kuongeza kuwa safari bado inaendelea na lengo ni kufika juu zaidi. - Spotileo ilimtafuta kuzungumzia ubora huo na yeye kusema kuwa imetokana na mapambano mazito aliyocheza mwaka jana na mabondia tofauti wa viwango vya juu. Takwimu za mtandao wa ngumi wa boxrec zinaonesha Class anashika nafasi ya kwanza Tanzania kati ya mabondia 90 wa uzito wa Super feather na nafasi ya 32 duniani kati ya mabondia 1,954. - Miaka miwili iliyopita hajapoteza pambano lolote liwe la ndani au la kimataifa.

Lilepo atua Kaizer Chief

Grody Lilepo amejiunga na Kaizer Chiefs ya South Africa akiungana na Kocha wa zamani wa Yanga Nassreddine Nabi Nassreddine anaenda kuifufua Kaizer Chief iliyopoteza makali kwa baadhi ya misimu nyuma.

Lava Lava kusepa WCB mwakani

Kwa mujibu wa taarifa kutoka moja kati ya vyanzo vya ndani ya record label kubwa barani Afrika WCB Wasafi Record ni kwamba nyota wa muziki wa record label hiyo Lava Lava mkataba wake na record label hiyo uko ukingoni,unaweza kuisha mwaka huu 2025au mwakani 2026. inadaiwa kuwa Lava lava alisaini mkataba wa kuwa msanii wa wasafi kati ya mwaka 2015 au 2016 Kisha akatambulishwa mwaka 2017, mkataba wake(contract duration) ulikua ni wa miaka kumi hivyo kama alisaini 2015 inamaanisha utaisha mwaka huu ila kama alisaini 2016 utaisha mwakani

Simba yaifanyia umafia mkubwa Yanga kwa Nzengeli

Timu ya soka ya Simba Sports Club imemalizana na timu ya Meniema Union kutoka DR Congo kuhusu mchezaji wao Max Mpia Nzengel. Mchezaji huyo yupo hapa nchini katika timu ya Yanga kwa mkopo na timu ya Simba Sports Club ndiyo chanzo cha mchezaji huyo kugoma kusaini mkataba mpya. Ndiyo maana kupitia Account yake Semaji (Ahmed Ally) kasema Kwamba Meniema Union ya Congo wamekula pesa yetu ndefu sana kwa hiyo mtachagua wenyewe,mtupe mchezaji wetu sasa hivi au tusubiri mwisho wa msimu

Ramovic amkataa Ikangalombo

Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic ameonyesha kutokuwa na imani yoyote kwa winga mpya Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’ baada ya kumchomoa katika kikosi cha wachezaji waliotakiwa kuanza jana dhidi ya Copco Wakati mashabiki wa Yanga wakiwa na hamu kubwa ya kumuona nyota mpya wa kikosi hicho, Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’ katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la (FA), dhidi ya Copco FC, mambo yamekuwa ni tofauti baada ya taaria kueleka kocha huyo hajaridhishwa kabisa na uwezo wake. Ramovic tayari ameomba mabosi wa Yanga kumletea winga mpya mwenye uwezo mkubwa wa kucheza mechi za Kimataifa katika dirisha kubwa la kuelekea msimu ujao.

Simba yaijibu Yanga, yapiga mtu 6-0

Timu ya Simba SC jioni ya leo imewajibu watani zao Yanga, baada ya kuilaza Kilimanjaro Worries ya Kilimanjaro mabao 6-0 mchezo wa mtoano kombe la CRDB uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Valentino Mashaka katika dakika ya kwanza aliifungia Simba kabla ya Ladack Chasambi dakika ya tatu kufunga la pili na Patrick Sebastian dakika ya nane alijifunga. Dakika ya 21 Joshua Mutale leo aliweza bao na Steven Mukwala dakika ya 48 akifunga bao la tano kabla ya Edwin Balua dakika ya 79 kufunga bao la sita

Novatus Dismas aing' arisha Goztepe

Kiungo Novatus Dismas amefunga bao moja kati ya mawili waliyofunga Göztepe kwenye mchezo wake dhidi ya Fenerbahçe wa ligi kuu ya Uturuki 'Super Lig'. Göztepe wamepoteza mchezo kwa mabao 3-2

Israel Mwenda mechi moja assist mbili

Kwa mara ya kwanza akicheza mchezo wake wa mashindano, beki wa kushoto Israel Mwenda jana aliweza kuhusika katika mabao mawili katika ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Copco FC ya Mwanza. Mwenda alijiunga na Yanga akitokea Singida Black Stars lakini kabla ya kwenda Singida, alikuwa anaichezea Simba SC, ametoa pasi za mwisho (assist mbili) well-done.

Joseph Guede apata timu Jordan

Mshambuliaji wa zamani wa yanga SC na Singida black Stars Joseph guede raia wa ivory coast amejiunga na klabu ya Al Wehdat ya Jordan Kwa mkataba wa miezi 6. Guede aliwahi kuichezea Yanga na anahusika kwenye mafanikio ya kufika robo fainali ya Ligi ya mabingwa Afrika ambapo goli lake dhidi ya CR Belouizdad ya Algeria liliiwezesha kutinga robo fainali. Pia aliwahi kuichezea Singida Black Stars kabla ya kuachana naye

Abdi Kassim "Babi" afichua maana ya jina lake la utani

ABDI Kassim anasema jina la 'BABI' siyo jina lake halisi isipokuwa lilitokana na kaka yake anayemtaja kwa jina la Shabaan kushindwa kutamka Abdi. "Badala ya kutamka Abdi alikuwa akiniita 'Babi" basi jina hilo lilishika kasi na kuenea kila mahali hadi leo hii."

Baleke ahitajika AmaZulu

Klabu ya Amazulu imeanza mazungumzo na TP Mazembe ili kuinasa saini ya mshambuliaji,Jean Baleke ambaye alikuwa akiitumikia Young Africans kwa mkopo. Amazulu wamehamia kwa Baleke baada ya kuikosa saini ya FRANK Ssebufu raia wa Uganda ambaye alikuwa akiitumikia New York Redbull II ya MLS. Inaelezwa kuwa TP Mazembe wanahitaji angalau Dolan 80,000 ili kumuachia jumla Jean Baleke ambaye aliwahi kuitumikia klabu ya Simba pia ya Tanzania.

Nyota wa kigeni Singida Black Stars avunja mkataba

Beki wa kushoto Benson Mangolo amefanikiwa kuvunja mkataba wake na Singida Black Stars. Mkataba huo ulikuwa unamalizika Juni, 2026. Kwasasa yupo kwenye hatua za mwisho za kujiunga na Mochudi Centre ya nyumbani kwao Botswana kwa mkataba wa miezi mitano.

Yanga yaitisha Kagera Sugar kwa bao 5-0

Mabingwa watetezi wa kombe la CRDB Benki au maarufu FA Cup, Yanga SC jioni ya leo imeanza vema kampeni yake ya kutetea ubingwa wake baada ya kuilaza Copco ya Mwanza mabao 5-0 uwanja wa KMC Complex uliopo Mwenge jijini Dar es Salaam. Mabingwa hao wakitoka kuondoshwa katika michuano ya Ligi ya mabingwa Afrika wiki iliyopita, wakipata bao la kwanza kupitia Shekhan Khamisi dakika ya 35, Prince Dube dakika ya 57 aliifungia Yanga bao la pili. Lakini dakika ya 67 Maxi Nzengeli alipachika bao la tatu kabla ya Duke Abuye dakika ya 77 kufunga bao la nne, na Mudathir Yahya dakika ya 84 kufunga idadi ya mabao kwa kuandika bao la nne. Kesho watani zao Simba watacheza na Kilimanjaro Worries katika uwanja huo huo kuwania kombe hilo la FA