Meneja Habari na Mawasiliano wa Simba SC, Ahmed Ally, ametoa ufafanuzi kuhusu kutokuwepo kwake kwenye hafla ya upangaji wa makundi ya AFCON 2025 inayotarajiwa kufanyika Januari 27 nchini Morocco. Akizungumza kupitia vyombo vya habari, Ahmed Ally alisema:
"Mimi CAF hawawezi kunifuata kwa sababu nina ratiba ya kuandaa timu kuelekea Robo Fainali, kwahiyo CAF wanaangalia nani hana kazi, ndiyo maana wanamualika yaani Jobless."
Kauli hii ilikuja baada ya taarifa kwamba Msemaji wa Yanga, Ally Kamwe, amepata mwaliko wa kuhudhuria hafla hiyo kutoka Shirikisho la soka la Afrika, CAF.
Ahmed Ally alisisitiza kuwa majukumu yake ndani ya Simba SC ni muhimu zaidi kwa wakati huu, hasa katika maandalizi ya timu kuelekea hatua ya Robo Fainali ya michuano inayoendelea