Ramovic amkataa Ikangalombo
Kocha Mkuu wa Yanga, Sead Ramovic ameonyesha kutokuwa na imani yoyote kwa winga mpya Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’ baada ya kumchomoa katika kikosi cha wachezaji waliotakiwa kuanza jana dhidi ya Copco
Wakati mashabiki wa Yanga wakiwa na hamu kubwa ya kumuona nyota mpya wa kikosi hicho, Jonathan Ikangalombo ‘Ikanga Speed’ katika mchezo wa Kombe la Shirikisho la (FA), dhidi ya Copco FC, mambo yamekuwa ni tofauti baada ya taaria kueleka kocha huyo hajaridhishwa kabisa na uwezo wake.
Ramovic tayari ameomba mabosi wa Yanga kumletea winga mpya mwenye uwezo mkubwa wa kucheza mechi za Kimataifa katika dirisha kubwa la kuelekea msimu ujao.