Sugu aanika utajiri wake
Joseph Mbilinyi 'Mr II Sugu' anasema utajiri wake wa sasa hauzidi Dola Milioni 10 sawa na Tsh Bilioni 26.
Sugu ameweka wazi hilo kufuatia taarifa ya chanzo kimoja mitandoni kuweka ana utajiri wa Dola Milioni 50 mpaka 150 zilizosababishwa na uwekezaji, muziki, biashara na masuala ya siasa.
"Nimeikuta hii ONLINE leo, nawashukuru ila naomba niseme wazi estimation yao sio ya kweli. My true WEALTH pamoja na my wifey @happiness_.mbilinyi as of now haizidi 10mil USD only" ameandika Sugu
