Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia Aprili, 2025

Fadlu achukizwa kufungwa na RSB Berkane mwaka 2022 akiwa na Orlando

Kocha mkuu wa Simba SC Fadlu David's amesema kufungwa na RSB Berkane katika fainali ya CAF Confederation Cup mwaka 2022 akiwa Orlando Pirates bado inamuuma hadi leo hiii. Tuliwatoa Simba Robo fainali tukawaangusha Al Ahli Tripoli nusu fainali lakini tukapoteza fainali dhidi ya RS Berkane Hivyo akikumbuka tukio hili anaumia sana.... Davids anasema ana iheshimu sana RS Berkane kutokana na ubora wake lakini wakati huu anataka kulipa kisasi akiwa na kikosi cha Simba SC, baada ya kupoteza taji la Shirikisho Afrika dhidi ya RSB Berkane akiwa na Orlando Pirates mwaka 2022." Fadlu David's: Kocha mkuu wa Simba

Al Ahly yamnyemelea Jose Riveiro

Klabu ya Al Ahly imeanza mazungumzo na Kocha José Riveiro ili kurithi mikoba ya Marcel Koller aliyeachana na Al Ahly hivi karibuni Hakuna ofa yoyote mezani kutoka klabu ya Young Africans SC, Riveiro ataachana na Orlando Pirates mwishoni mwa msimu huu Kocha José Riveiro anahusishwa kuhitajika na Young Africans kuelekea msimu ujao ijapo hakuna ofa rasmi kutoka kwa giants hao wa Tanzania.

TFF, Bodi ya Ligi zafikishwa mahakamani

Shirikisho la Mpira Nchini Tanzania pamoja na Bodi ya Ligi Kuu Tanzania Wameitwa mbele ya Jaji wa Mahakama Kuu (masijala ndogo ya Dar Es Salaam) Mh. Jaji E. Mkwizu tarehe 2 Mei 2025 saa 1:30 asubuhi bila kukosa kwa ajili ya kusikiliza madai ya shabiki wa mpira wa miguu kutoka Iringa Mjini Dk. Samweli Marwa. . Kwenye shauri hilo TFF ndiye mdaiwa wa kwanza na Bodi ya Ligi ndiye mdaiwa wa pili na madai hayo yanahusiana na kuaihirishwa kwa mechi ya watani wa jadi tarehe 8 Machi 2025.

Uwanja wa Uhuru zamani Taifa nao kufungwa taa

Uwanja wa Uhuru (zamani Taifa au shamba la bibi) uliopo jijini Dar es Salaam unaendelea kuboreshwa ili uwe uwanja wa kisasa wenye hadhi ya kutumika mashindano makubwa ya kimataifa. Vile vile uwanja huo utaongezewa jukwaa, utawekewa viti vipya, utawekewa taa za kisasa na maboresho mengine yatakuwa sehemu ya kubadiliahia nguo pamoja na sehemu ya vyoo.

Rasmi, Olympique de Marseille ya Ufaransa yajitosa mazima kwa Mzize

Klabu ya Olympique de Marseille kutoka Ufaransa inamfatilia Mshambuliaji Clement Mzize (21) wa Young Africans ili kupata saini yake katika dirisha kubwa la usajili Marseille imetenga ofa USD 1.8m (Tshs 5 bilioni) ili kupata huduma ya mchezaji huyo ambaye amekuwa na kiwango bora sana katika klabu ya Young Africans kwa misimu miwili mfululizo Marseille it has put the number of three players to register one in the next transfer window including the name of Clement Mzize.

Yanga kumtema Kennedy Musonda

Klabu ya Young Africans imempa taarifa Mshambuliaji Kennedy Musonda (30) kuwa haitaendelea nae baada ya msimu huu kumalizika na mchezaji amepokea taarifa hiyo Menejimenti ya Kennedy Musonda inafanya mazungumzo na Al Ittihad ya Libya na Power Dynamos ili ajiunge nayo, Menejimenti ya mchezaji huyo inamtafutia klabu mojawapo katika klabu hizi mbili Mchakato wa kumtafutia timu Kennedy Musonda unaendelea kwa Menejimenti ya Kennedy Musonda baada ya kumalizana na Young Africans kwa kila kitu.

Yanga yaifuata JKU fainali ya Muungano

Mabingwa wa zamani wa kombe la Muungano, Yanga SC wamefanikiwa kutinga hatua ya fainali baada ya usiku huu kuifunga Zimamoto Kwa mikwaju ya penalti 3-0 kufuatia sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Gombani Pemba. Yanga walitangulia kupata bao kupitia Maxi Nzengeli dakika ya 28 kabla ya Zimamoto kusawazisha dakika ya 70 kupitia Said Mwinyi, mpira ulimalizika baada ya dakika 90 na wakaenda kwenye changamoto ya penalti. Yanga walipata penalti tatu na Zimamoto walipoteza tatu na mpira ukamalizwa, penalti ya ushindi ilipigwa na Clement Mzize, Yanga sasa watakutana na JKU Alhamisi kilele cha sherehe za Muungano .

Yanga kuachana na Sportpesa

Klabu ya Yanga ipo kwenye hatua za mwisho za kukamilisha makubaliano na mdhamini mpya wa klabu hiyo atayekaa kifuani kwenye Jezi zao kwa fedha itayoweka rekodi nchini. Taarifa zinaeleza kuwa Sportpesa hatokaa tena kifuani, atakaa mgongoni mwa Jezi kumpisha mdhamini mkuu mpya.

Msimu ujao Mzize kucheza Ligi Kuu Ufaransa

Meneja wa Habari wa klabu ya Yanga, Ally Kamwe amethibitisha kuwa mshambuliaji, Clement Mzize atachezea Ligi Kuu Ufaransa msimu ujao ingawa hajabainisha ni timu gani kinara huyo wa magoli kwenye Ligi Kuu bara atachezea. Ally Kamwe amebainisha kuwa Yanga Sc itapata bilioni 5 kwa mauzo ha nyota huyo ingawa ameshindwa kuitaja timu timu inayomtaka "Siwezi kuitaja timu lakini kuna mazungumzo na Timu ya Ufaransa, Yanga tunapata bilioni 5, msimu ujao Mzize atakuwa Ligi Kuu Ufaransa kama kuna timu ina bilioni 5 ilete,” — Ali Kamwe

Yanga na Kelvin Nashon kuteta upya

Klabu ya Young Africans SC mwanzoni mwa wiki ijayo itaanza mazungumzo rasmi tena na kiungo wa ulinzi kutoka Singida Black Stars, Kelvin Nashon ili kujiunga nao kuelekea msimu ujao Kelvin Nashon anahitajika Young Africans SC ili kuongeza nguvu akishirikiana na kiungo wa ulinzi Khalid Aucho ambaye amekuwa akipata majeraha ya mara kwa mara, Young Africans inaamini Nashon ataongeza kitu kikubwa katika eneo la ulinzi kutokana na kipaji chake Young Africans SC ilistisha mchakato wa kumsainisha Kelvin Nashon katika dirisha dogo la uhamisho kwakuwa klabu ilikuwa katika kipindi kigumu cha mwenendo wa matokeo uwanjani

Wallace Karia aongoza warsha ya FIFA, UEFA NA CAF

Rais wa TFF, Wallace Karia ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Warsha ya FIFA inayohusisha Nchi Wanachama wa UEFA na CAF inayofanyika Vienna, Austria. Nchi zinazohudhuria kwenye Warsha hiyo ya kuimarisha maendeleo ya soka duniani ni Finland, Moldova, Wales, Austria, Georgia kutoka UEFA na Gabon, Morocco, Senegal, Tanzania na Cameroon kutoka CAF

Straika Stellenbosch aipongeza Simba kutinga fainali

‎Straika wa Stellenbosch, Andre Ernest de Jong (jezi namba 18) raia wa New Zealand ‎amewapongeza Simba kutinga fainali na kuimwagia sifa zaidi safu ya ulinzi akimtaja Abdlurack kama ni moja ya walinzi alikuwa kikwazo kwake. ‎ ‎”Simba wana timu nzuri, safu yao ya ulinzi nzuri zaidi naweza kusema kwenye haya mashindano tangu mwanzo wao na RS Berkane walikuwa bora mno kuliko timu zote, yule jezi namba nne (Hamza) ni kati ya mabeki bora Afrika kwa sasa.” ‎ ‎

Pongezi za Rais Samia na mashabiki wao zinawatosha- Mangungu

Mwenyekiti wa Klabu ya Simba SC, Murtaza Mangungu amesema hawahitaji pongezi toka kwa taasisi yoyote nchini zaidi ya pongezi za Rais Samia na mashabiki wao zinawatosha. "Inabidi Simba SC tueleweke vizuri , hatuhitaji pongezi za kiongozi wa taasisi wa timu nyingine kuja kutupongeza sisi kuingia fainali Shirikisho Afrika " " Pongezi za Mh Rais na Mashabiki wetu wa Simba SC zinatosha sana kwetu viongozi katika kesi hii ". - Murtaza Mangungu, Mwenyekiti wa klabu ya Simba SC akiongea baada ya kuwasili Tanzania.

Simba walivyotua Dar leo

Kikosi cha Wanafainali wa Kombe la Shirikisho Barani Afrika,Simba SC wametua Nchini wakitokea Afrika Kusini walikoenda kuiwakilisha nchi kwenye michuano ya Kimataifa kisha wakafuzu hatua ya Fainali ya Mashindano hayo.

Azam FC yatolewa kombe la Muungano

Timu ya Azam FC ya jijini Dar es Salaam imetolewa katika michuano ya kombe la Muungano baada ya kufungwa mabao 2-1 na JKU ya Zanzibar uwanja wa Gombani Pemba. Huu ni msimu mbaya kwa Azam FC kwani wameambulia patupu katika mashindano yote waliyoshiriki. Neva Adelin dakika ya 50 aliifungia JKU bao la kwanza kabla ya Freddy Suleiman kufunga la pili, Yeison Fuentes aliipatia Azam FC bao la kufuatia machozi dakika ya 15 akitangulia kufunga, dakika ya 90 Abdulhalim Masoud wa JKU alioneshwa kadi nyekundu, JKU wameingia fainali na sasa wanasubiri mshindi kati ya Yanga na Zimamoto kesho. .

Lusajo Mwaikenda na rekodi ya beki wa mabao mengi Ligi Kuu bara

BEKI wa Azam FC, Lusajo Mwaikenda amevunja rekodi ya msimu uliopita ya mabeki waliofunga mabao mengi zaidi katika Ligi Kuu, baada ya nyota huyo kufunga moja na kufikisha matano katika ushindi wa kikosi hicho wa 4-2, dhidi ya Kagera Sugar. Lusajo alifunga bao hilo dakika ya 42, akiunganisha kwa kichwa kona iliyopigwa na Abdul Suleiman ‘Sopu’ na kuisawazishia Azam baada ya Hijjah Shamte kuitanguliza Kagera dakika 26, kisha Idd Seleman ‘Nado’ kupachika la pili dakika ya 58. Kagera ilijibu mapigo na kusawazisha dakika ya 60 kupitia kwa Kassim Fekha, huku Nassoro Kapama akijifunga dakika ya 82 katika harakati za kuokoa mpira wa Lusajo na kuipa Azam bao la tatu, kabla ya Mcolombia Jhonier Blanco kufunga bao moja kali la nne katika dakika ya 87 ya mchezo. Kitendo cha Lusajo kufunga bao moja kimemfanya kufikisha mabao matano ya Ligi Kuu msimu huu na kuivunja rekodi ya msimu uliopita, ambapo beki aliyekuwa na mabao mengi zaidi alikuwa ni Derrick Mukombozi wa Namungo FC aliyefunga manne. Mbali n...

Duke Abuye naye kutimka Yanga

Kiungo mshambuliaji wa Yanga Mkenya "Duke Abuya"ambaye mkataba wake unakwishwa mwishoni mwa msimu huu amepokea ofa kutoka nchini Algeria klabu ya JS Kabylie. Hadi sasa hakuna mazungumzo yoyote kati ya menejimenti ya Mchezaji na Uongozi wa Yanga kuhusu mkataba mpya.Duke Abuya alisajiliwa msimu huu 2024-2025 Kwa mkataba wa mwaka mmoja akitokea Singida Big Star.

Pacome Zouzoua aipa taadhali Yanga imuuze fasta

Taarifa kutoka kwenye chanzo changu Cha kuaminika zinadai Paccome Zouzoua ana offer ya Al Ahly hivyo amewaambia Yanga wachukue hela sasa hivi au ataondoka Bure msimu ujao maana hataongeza Mkataba mpya. Al Ahly SC imetuma Ofa ya 1.5Bilioni za Kitanzania kwenda Yanga ili kupata huduma ya mchezaji wao nyota Pacôme Zouzoua. Pacôme Zouzoua Amekubali kujiunga na Al Ahly SC atakuwa akilipwa 126 Milioni za Kitanzania.

Simba ruksa kuutumia uwanja wa Mkapa fainali

Simba SC imehakikishiwa kuutumia uwanja wa Benjamini Mkapa, kwenye mchezo wa Mkondo wa pili wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika 2024/25 dhidi ya RS Berkane ya Morocco. Simba atacheza mechi ya kwanza Morocco May 17, kisha mchezo wa marejeano Dar es salamaa, May 25,2025.

Fadlu akataa sherehe Simba mpaka ubingwa

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Simba Sports Club Fadlu David's amewaambia vijana (wachezaji ) . kwamba hatakiĺ kusikia sherehe aina yoyote baada ya timu hiyo kutinga fainali ya Shirikisho Afrika. Fadlu David's amewaambia wachezaji wake kwamba.kama ni sherehe basi ziishie kwenye nyumba vya kubadilishia nguo tu.(dressing room) Baada ya kutoka (dressing room )kwenye vyumba vya kubadilishia nguo.moja kwa moja waanze maadalizi ya mchezo RS Berkane May 17 nchini Morocco.

RS Berkane yaitupa nje CS Constantine, sasa kuumana na Simba fainali

Klabu ya RS Berkane kutoka Morocco imefanikiwa kafuzu hatua ya Fainali ya CAF Confederation Cup kwa kuiondosha Klabu ya Cs Constantine ya Algeria kwa matokeo ya jumla ya Magoli 4-1 Rs Berkane itakutana na Simba SC ya Tanzania kwenye hatua ya Fainali ambapo Fainali ya kwanza itachezwa Morocco na Fainali ya pili itachezwa Tanzania.

Diana Lucas apiga hat trick Uturuki

Nyota wa Tanzania Diana Lucas amefunga mabao matatu (hat-trick) wakati timu yake ya Trabzonspor ikipata ushindi wa mabao 17-0 dhidi ya Cekmekoy kwenye mchezo wa Ligi Kuu ya Uturuki

Simba yaandika rekodi, yatinga fainali, Rais Samia awapongeza

Wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya kombe la Shirikisho barani Afrika, Simba SC imeandika rekodi baada ya kufanikiwa kutinga fainali kufuatia sare tasa 0-0 dhidi ya Stellenbosch ya Afrika Kusini. Kwa matokeo hayo Simba inafuzu fainali kufuatia ushindi wa 1-0 walioupata jijini Dar es Salaam katika uwanja wa Mkapa. Simba sasa inasubiri mshindi wa jumla kati ya CS Constantine ya Algeria na RS Berkane ya Morocco ambao wanachuana usiku huu. Mchezo wa leo uliomalizika kwa sare tasa, VAR ikikataa bao la Stellenbosch ikidai mchezaji aliyetoa assist ya bao aliotea. Wakati huo huo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan ameipongeza timu ya Simba kwa kuingia Fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuitoa Stellenbosch jioni ya leo nchini Afrika Kusini. “Pongezi za dhati kwa Klabu ya Simba kwa ushindi katika mchezo wa Mashindano ya Kombe la Shirikisho la Soka Afrika (CAF Confederation Cup), na kuandika historia ya kufika fainali ya mashindano haya,” amesema Ra...

Al Ahly yamfuta kazi kocha wake mkuu

Klabu ya Al Ahly ya Misri imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha wao mkuu Marcel Kohler mara baada ya Klabu hiyo kutupwa nje kwenye michuano ya CAFCL hatua ya Nusu fainali dhidi ya Mamelodi Sundown. Bao la kujifunga wenyewe la Al Ahly liliiwezesha Mamelodi Sundown's kusawazisha na kuwa sare ya 1-1 lakini Mamelodi inabebwa na Sheria ya goli la ugenini.

Yacouba Sogne uso kwa uso na Seleman Mwalimu Morocco

Katika jiji la Casablanca, Morocco, njia za wapiganaji wawili wa kandanda zimevuka. Yacouba Sogne, mshambuliaji wa Tabora United, akiwa katika safari ya uponyaji, amekutana na Seleman Mwalimu Gomez wa Wydad Athletic. Licha ya tofauti ya vilabu na Nchi, kinachowaunganisha ni kitu kimoja: mapenzi ya mpira wa miguu. Soka sio tu mchezo wa ushindani — ni lugha ya ulimwengu, ni daraja kati ya mioyo, ni sauti ya mshikamano bila mipaka. Katika muktadha huu, soka imethibitisha tena dhamira yake ya kuwa zaidi ya mchezo — kuwa njia ya kuunganisha watu, tamaduni na matumaini. Soka hujenga urafiki, huponya nafsi, na huandika hadithi zinazovuka mipaka ya muda na mahali.

Yanga waifuata Azam nusu fainali kombe la Muungano

Mabingwa wa Tanzania bara, Yanga SC usiku huu katika uwanja wa Gombani Pemba, imetinga nusu fainali ya kombe la Muungano baada ya kuilaza KVZ mabao 2-0. Alikuwa Stephanie Aziz Ki kuitanguliza Yanga kwa bao lake la kwanza dakika ya 27 kabla ya Denis Nkane dakika ya 84 kufunga bao la pili ambapo sasa ni kama wameifuata Azam FC nusu fainali.

Valentine Nouma aomba kuondoka Simba

Taarifa kutoka chanzo cha kuaminika sana kuhusu mlinzi wa kushoto wa Simba SC Valentine Nouma raia wa Burkina Faso ameuomba uongozi wa Simba kumuacha huru mwishoni mwa msimu huu. Huku taarifa zikieleza kwamba sababu za kuondoka kwa nyota huyo ni kukosa nafasi kwenye kikosi cha kwanza ndani ya timu ya Simba ambapo nafasi yake ndiyo anayocheza Mohamed Hussein Tshabalala

Aigle Noir mabingwa Ligi Kuu Burundi

Klabu ya Aigle Noir CS imeibuka Bingwa wa Ligi Kuu Burundi, baada ya kutoka sare ya 0-0 dhidi ya Royal Vision 2026 zikiwa zimebaki mechi mbili ili Ligi iweze kutamatika. Imetwaa Kombe hilo baada ya Bumamuru FC iliyokuwa ikikimbizana na Aigle Noir CS kupokea kichapo cha mabao 2-0 kutoka kwa Musongati FC ya mkoani Gitega. Aigle Noir Club Sportif imetangazwa Bingwa ikiwa na pointi 8 mbele ya Bumamuru FC. Baada ya miaka 6, Fighters wanashinda taji lao la pili la Ubingwa wa Ligi Kuu katika historia yao. Mechi ambazo zimebaki kwa Aigle Noir CS kabla ya Ligi Kuu kumalizika ni dhidi ya Rukinzo FC wiki ya 29 na Inter Stars wiki ya 30.

Maelfu wamzika Papa Francis

KIONGOZI wa Kanisa Katoliki, na Rais wa Vatican, Papa Francis amezikwa katika Kanisa kuu la Santa Maria Maggiore mjini Roma baada ya ibada ya mazishi iliyohudhuriwa na watu 250,000 katika uwanja wa St. Peter’s mjini Vatican. Mbali na viongozi wa Dunia, hafla ya mazishi ya Papa Francis imehudhuriwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Philip Isdor Mpango ambaye aliambatana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi Mahmoud Kombo pamoja na watu muhimu kama vile Rais wa Marekani Donald Trump, Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Waziri Mkuu wa Uingereza, Keir Starmer. Sherehe za mazishi zilianza saa 5:00 asubuhi kwa saa za Afrika Mashariki, huku mwili wa Papa Francis ukibebwa kwenye uwanja wa Kanisa kuu la Mtakatifu Petro ambapo baada ya sherehe hizo, Kardinali Giovanni Battista Re alitoa hotuba akisisitiza uhusiano wa Papa na watu na umuhimu anaoupa kwa amani huku akinukuu maneno ya Papa, “Jenga madaraja, sio kuta.” Baada ya sherehe, mwili wa ...

Fadlu azitosa ofa mbili za Orlando na Raja kisa Simba

Kocha mkuu wa timu ya soka ya Simba Sports Club.Fadlu David's amepiga chini ofa mbili mezani kwake. Moja Raja Casablanca kutoka nchini Morocco.pamoja na timu ya soka ya Orlando Pirates kutoka Afrika Kusini. Fadlu akiwaambia kwamba yeye hawezi kuondoka katika timu ya soka ya Simba Sports Club kabla ya mkataba wake kuisha.