Klabu ya Al Ahly ya Misri imetangaza rasmi kumfuta kazi kocha wao mkuu Marcel Kohler mara baada ya Klabu hiyo kutupwa nje kwenye michuano ya CAFCL hatua ya Nusu fainali dhidi ya Mamelodi Sundown.
Bao la kujifunga wenyewe la Al Ahly liliiwezesha Mamelodi Sundown's kusawazisha na kuwa sare ya 1-1 lakini Mamelodi inabebwa na Sheria ya goli la ugenini.