Tanzania kuandaa AFCON U20 Septemba


Kura za michuano ya kufuzu AFCON kwa vijana chini ya umri wa miaka 20 kanda ya CECAFA zimepigwa rasmi mjini Kigali, huku Tanzania ikiwa mwenyeji wa michuano hiyo mikubwa itakayopigwa mwezi Septemba.

Tanzania imepangwa pamoja na Ethiopia na Rwanda, ikiwa ni kundi lenye ushindani mkubwa wa Afrika Mashariki.

Kundi B linawakutanisha Uganda, Sudan, na Djibouti, wakati Kundi C linajumuisha South Sudan, Kenya, na Burundi.

Vinara wa makundi yote matatu pamoja na mshindi wa pili aliye na matokeo mazuri zaidi watatinga hatua ya nusu fainali. Timu mbili za mwisho zitakazochuana kwenye fainali ndizo zitakazowakilisha kanda ya CECAFA katika michuano ya AFCON U-20 2026.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI