Ally Kamwe akanusha Yanga kufungiwa na FIFA kusajili

Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Young Africans SC, Ally Kamwe, amekanusha madai yanayoelezwa kuwa klabu hiyo imefungiwa kufanya usajili kwa kipindi cha misimu mitatu mfululizo.

Kamwe amesema Yanga SC bado inaendelea na shughuli zake za usajili, huku akisisitiza kuwa taarifa za usajili wa klabu hiyo zimewasilishwa na zinaonekana kwenye mfumo husika.Kauli hiyo imekuja wakati ambapo taarifa kuhusu hali ya usajili wa Yanga zimeendelea kusambaa na kuzua mjadala miongoni mwa mashabiki na wadau wa soka nchini.

Hata hivyo, Kamwe amesema kwa maelezo zaidi kuhusu suala hilo, wadau wanapaswa kuwasiliana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), akieleza kuwa TFF ndiyo yenye taarifa na majibu rasmi kuhusu hali ya usajili wa klabu hiyo.


Machapisho maarufu kutoka blogu hii

FIFA yatoa orodha ya vilabu bora duniani, Simba na Yanga zachuana vikali

Kocha Simba anataka wachezaji wapya watano

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI