Yanga, Sportpesa wateta
Mapema asubuhi ya leo, Uongozi wa YANGA SC ukiongozwa na Rais Eng. Hersi Said ulifanya kikao na Mdhamini Mkuu wa Klabu yetu, Kampuni ya SportPesa na kujadili mambo mbalimbali ya kimkataba na mahusiano ya pande zote mbili.
Upande wa Kampuni ya SportPesa uliwakilishwa na Tarimba Abbas, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi, Allan McTavish, Mkuu wa Kimataifa wa Udhamini na Sabrina Msuya ambaye ni Mshauri wa Udhamini Mahusiano na Serikali.






