Singida Black Stars yaja na mzungu
Klabu ya Singida Black Stars imemtambulisha rasmi kiungo mshambuliaji Marcel Canad kuwa sehemu ya kikosi kitakachoiwakilisha klabu hiyo katika msimu wa 2026/27.Marcel, mwenye umri wa miaka 28, anatajwa kuwa miongoni mwa wachezaji wanaotarajiwa kuongeza nguvu na ubunifu katika eneo la kiungo cha ushambuliaji la Singida Black Stars.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa, Marcel amewahi kuwa sehemu ya mfumo wa Borussia Mönchengladbach, klabu inayoshiriki Ligi Kuu ya Ujerumani (Bundesliga), katika kipindi cha mwaka 2014 hadi 2017.Usajili wake unaongeza hamasa kwa mashabiki wa Singida Black Stars, ambao sasa wanaanza kuona picha ya kikosi kitakachopambana kwenye msimu mpya.
