Prince Dube atambulishwa Zimbabwe
Mshambuliaji wa kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube, ametambulishwa rasmi kama mchezaji mpya wa Hard Rock FC ya nchini Zimbabwe, akianza rasmi safari mpya ya soka katika taifa lake.
Kwa mujibu wa taarifa hizo, Dube ameamua kujiunga na Hard Rock FC licha ya kuripotiwa kuvutiwa na klabu kadhaa, zikiwemo Young Africans SC (Yanga), Al Ahly Benghazi ya Libya na Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini.
Uamuzi huo unahitimisha uvumi wa muda mrefu kuhusu hatma ya mshambuliaji huyo baada ya kumalizika kwa mkataba wake na Yanga SC.Tunamtakia Prince Dube kila la heri katika changamoto mpya ya maisha yake ya soka.
