Hatuna habari na Fadlu- AliKamwe
Klabu ya Young Africans SC kupitia kwa Afisa Habari wake, Ally Kamwe, imetolea ufafanuzi wa haraka uvumi unaoendelea mitandaoni kuhusu mchakato wa kusaka kocha mpya.
Kamwe ameweka wazi kuwa uongozi haujafanya mazungumzo yoyote na kocha Fadlu Davids na kuwataka mashabiki kupuuza taarifa zote za usajili zinazosambazwa kwa sasa, kwani nguvu zao zote zimeelekezwa kwenye mchezo wa kesho wa kusaka ubingwa.
Ujumbe wake kamili unasomeka hivi:"Uongozi wa YANGA SC haujafanya mazungumzo Yoyote wala hauna mpango wa kumuajiri Kocha Fadlu Davis ..
Ni vile tu watu wanapitia kipindi kigumu kupata Breaking News za YANGA ndio maana wanaanzisha jambo la kulimaliza wenyewe juu kwa juu
Kwenu Wananchi, Habari sahihi za YANGA SC mtazipata kupitia YANGA APP na Kurasa zetu za Mitandao ya Kijamii za klabu ya YANGA
Kipindi hiki, Habari yoyote ya Usajili wa Wachezaji au Kocha utakaousoma huku Mitandaoni, Ni UZUSHI na UONGO.
Kwa sasa, Focus yetu Yote iko kesho. Twendeni Uwanjani Tukapambanie UBINGWA wetu wa 5 wa Ligi Kuu In Shaa Allah."
