Tuko nyuma ya 2-0 kwa Al Ahli Tripoli- Ahmed Ally
Meneja wa habari na Mawasiliano wa Simba SC Ahmed Ally amesema kimuonekano Simba SC ni kama imefungwa mabao 2-0 kwa sababu wapinzani wao waliwazidi kwenye maeneo mawili. "Mpaka sasa tupo nyuma goli 2-0 dhidi ya mashabiki wa Al Ahli Tripoli. Goli la kwanza kuujaza uwanja wao wote kwa mashabiki 50,065. Hili kwetu ni deni na sisi kuujaza. Sina hofu na hilo kujaza uwanja wa Mkapa. Wao walijaa na sisi tunapaswa kujaa. Goli la pili mashabiki wote kuvaa jezi za timu yao, na hilo tuna wajibu wa kwenda kusawazisha. Kila Mwanasimba atakayekuja uwanjani anatakiwa kuvaa jezi mpya ya msimu hii.” “Kwa kutambua kwamba tunapaswa kuvaa jezi za aina moja, mdhamini wetu wa jezi amepunguza bei kwa punguzo maalumu. Jezi zitauzwa Tsh. 30,000 na zinapatikana kwenye maduka ya Sandaland The Only One lakini pia kwa atakayekuja uwanjani na kununua jezi yake ya Tsh. 30,000 atampa zawadi ya tiketi ya mchezo bure.” “Tunapohimiza watu wavae jezi, tunahimiza watu wavae jezi orijino. Tuseme wazi kwamba tayari tun