Rais wa Ghana Akufo Addo ameamrisha kukamatwa mwenyekiti wa Shirikisho la kandanda la Ghana Kwesi Nyantekyi, ambaye pia ni makamu wa Rais wa kwanza wa Shirikisho la kandanda barani Afrika, CAF.
Hatua hiyo inafuatia makala moja ya uchunguzi ambayo inamuhusisha Kwesi Nyantekyi na vitendo vya ulaghai, inadaiwa kuwa Kwesi alitumia jina la Rais wakati wa kutekelez ulaghai huo.
Uchunguzi huo uliofanywa na mwandishi wa habari maarufu Anas Aremeyaw Anas uliwasilishwa kwa Rais wa nchi, uchunguzi huo pia unadaiwa kufichua vitendo vya ufisadi miongoni mwa maofisa wengine wa Shirikisho la kandanda nchini Ghana.
Video inayoonyesha ulaghai huo imepangwa kuonyeshwa kwa umma mnamo tarehe 6 mwezi ujao, Kwesi Nyantekyi amekuwa mwenyekiti wa Shirikisho la kandanda nchini Ghana tangu mwaka 2005 hajatamka lolote