Ruka hadi kwenye maudhui makuu

KISPOTI:

MIKONO YA NDUDA INALALAMIKA.
Na Prince Hoza
MASHABIKI na wapenzi wa Simba SC kuna wakati hawaeleweki kabisa, wao wanapenda starehe tu, shida ama taabu kwao si rafiki kabisa na hawataki kusikia kitu kama hicho, ukiwa na shida zako hawana habari na wewe wao wanachapa mwendo, hao ndio mashabiki wa Simba ambao wanacheka kwa dharau.
Wanacheka kwa dharau kwa sababu timu yao kwa sasa ipo katika ubora wa hali ya juu, kikosi cha Simba kinaendeleza kutoa dozi kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara.
Simba ilianza ligi kwa kishindo baada ya kuichapa Ruvu Shooting ya Mlandizi Pwani mabao 7-0 kabla haijalazimishwa sare isiyo ya mabao 0-0 na Azam FC ikiwa ni mechi yake ya kwanza kucheza ugenini, mechi hiyo ilipigwa uwanja wa Azam Complex, Chamazi nje kidogo ya Dar es Salaam.
Lakini mwishoni mwa wiki iliyopita, Simba iliivulumishia Mwadui FC ya Shinyanga mabao 3-0 mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru Dar es Salaam, ushindi huo umeiwezesha Simba kufikisha pointi 7 na ikikamata nafasi ya pili nyuma ya vinara wa ligi hiyo Mtibwa Sugar wenye pointi 9, baada ya kushinda mechi zote tatu ilizocheza.
Lakini Simba ndio timu yenye mabao mengi zaidi, ikifunga mabao kumi huku mchezaji wake Emmanuel Okwi raia wa Uganda akiongoza kwa ufungaji wa magoli, mpaka sasa Okwi amefunga magoli 6 na wanaomfuatia kwa vyovyote watakuwa wamefunga magoli mawili.
Hapo utaona tu jinsi mashabiki wa Mnyama wanavyocheka kwa dharau, hawama habari kwani timu yao inawapa raha, watani zao Yanga wako taabani kwani hadi sasa wamecheza mechi tatu kama ilivyo Simba lakini wameambulia pointi tano, Yanga wameambulia sare mechi mbili na wakishinda mechi moja tu.
Mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, walianza ligi kwa kushikwa shati na Wanapaluhengo, Lipuli ya Iringa wakifungana bao 1-1 mchezo uliofanyika uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam, Yanga ilisawazisha goli ikitaka kulala mbele ya vijana hao wanaonolewa na kiungo wa zamani wa Simba, Seleman Matola "Veron".
Yanga ikapata ushindi wake wa kwanza mjini Njombe baada ya kuilaza Njombe Mji FC bao 1-0 bao ambalo walilipata kwa mpira wa faulo likifungwa kistadi na Ibrahim Ajibu, mabingwa hao wakabanwa mbavu na Majimaji katika mchezo mwingine wa ligi uliofanyika katika uwanja wa Majimaji mjini Songea, Jumamosi iliyopita.
Yanga na Majimaji zilifungana bao 1-1, hivyo wanarejea Dar es Salaam na pointi nne walizozipata huko Nyanda za juu kusini, watani zao Simba wanacheka kwa dharau hasa baada ya Yanga kuboronga kiasi hicho, safu ya ushambuliaji ya Yanga hadi sasa imefunga mabao matatu tu huku yakiwa yameachwa mbali na mchezaji mmoja wa Simba, Emmanuel Okwi mwenye mabao sita peke yake.
Simba sasa wanajiandaa kuifuata Mbao FC jijini Mwanza katika mwendelezo wa Ligi Kuu Bara, hiyo ndiyo Simba, Lakini kwa upande mwingine kuna changsmoto zake toka kwa mashabiki wake, mashabiki wake hawana simile, Timu yao ikitokea kufanya vibaya hata kwa kutoka sare lawana huanzia hapo.
Hivi karibuni ililazimishwa sare tasa na Azam FC ya 0-0 katika uwanja wa Azam Complex, mashabiki wa Simba  walianza kumlakamikia kocha wao Mcameroon Joseph Omog wakidai ameshindwa kukinoa kikosi hicho, mashabiki hao walikuwa wakimtaka Jonas Mkude.
Hata  kwenye mchezo wa jana dhidi ya Mwadui, mashabiki wa Simba walikuwa wakimlaumu Omog kwa kitendo chake cha kuwatoa Shiza Kichuya na Nicolaus Gyan, mashabiki hao walitaka John Bocco "Adebayor" atolewe, lakini Bocco alipofunga goli la tatu ambalo lilikuwa maridadi ambalo liliwanyamazisha mashabiki hao.
Mechi zote hizo tatu, Simba imemwanzisha langoni kipa wake Aishi Manula, na kipa mwingine Emmanuel Mseja amekuwa akianzia benchi, lakini Simba msimu huu imesajili makipa  watatu akiwemo na Said Mohamed Nduda, Nduda alikuwa kipa wa kwanza wa Mtibwa Sugar ya Turiani mkoani Morogoro.
Kwa bahati mbaya kipa huyo ni majeruhi, Nduda aliumia mazoezini kule Zanzibar wakati Simba ilipoenda kuweka kambi kujiandaa na mchezo wake wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga, Nduda alisajiliwa na Simba baada ya kuibuka kipa bora wa michuano ya Cosafa Castle Cup iliyofanyika nchini Afrika Kusini.
Umuhimu wa Nduda katika kikosi cha Simba kwa sasa hauonekani kabisa, hata viongozi wa timu hiyo kwa sasa wanasikilizia tu, awali kipa huyo ilikuwa asafirishwe haraka kwenda India kufanyiwa matibabu, lakini safari hiyo haikuwemo na kilichobakia kwao ni kutoa maelezo kwamba watampeleka India.
Mashabiki wa Simba hawana habari naye kwa sababu kipa Aishi Manula hajaruhusu hata bao moja langoni kwake, unamuwazaje kipa mwingine kwa mfano, Said Mohamed Nduda kwa vyovyote anasubiri safari, mikono yake inalalamika, na inalalamika kwa sababu achezi.
Lakini mashabiki wa Simba wataupigia kelele uongozi wao kuhusu kuchelewesha matibabu ya kipa huyo iwapo tu Aishi Manula atafungwa magoli ya kizembe, wako wapi Vincent Angban na Daniel Agyei, ukipata majibu walipo basi Simba isizuge kwa Said Mohamed na afanyiwe wepesi ili atibiwe haraka na arejee kazini.
Said Mohamed ajira yake mpira, kucheza kwake ndio kunaboresha kiwango chake, anavyozidi kukaa nje ndipo umahiri wake utakapoanza kushuka na mwishowe tutamuona kipa huyo akiangukia vitimu vya madaraja ya chini, Afya yake ni muhimu sana kwa sasa kwani nina uhakika hajaenda kutibiwa
Said Mohamed Nduda

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC