Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Hii ndiyo historia kamili ya Yanga SC iliyotimiza miaka 80 ya kuzaliwa kwake.



YANGA SC siku ya Idd pili itasherehekea miaka ya 80 ya kuzaliwa kwake, pia itasherehekea ubingwa wake wa 25 iliyoutwaa msimu uliomalizika mwaka huu.

Katibu mkuu wa Yanga Dk Jonas Toboroha aliiambia Afrika Soka kuwa sherehe hizo sasa zitafanyika siku ya Idd pili baada ya kukubali kuzisogeza mbele, awali sherehe hizo zilikuwa zifanyike jumamosi iliyopita ya tarehe 27 Juni mwaka huu.

Siku hiyo kulipangwa kufanyika kwa burudani kadhaa kutoka kwa wanamuziki wetu, pia mgeni wa heshima ilikuwa awe rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Kikwete ambaye pia ni mpenzi mkubwa wa Yanga.


Bendi ya Yamoto, Msondo Ngoma, Lady Jaydee na Msagasumu walialikwa kutoa burudani siku hiyo ya kusherehekea miaka 80 ya Yanga, lakini pia kuna uwezekano mkubwa wakawepo siku hiyo ya Idd pili ambapo sherehe izo zitafanyika.

Sherehe hizo zitafanyikia makao makuu ya Yanga Jangwani, Wanayanga wote watajumuika, awali baadhi ya wapenzi na mashabiki wa Yanga waliokuwa kwenye mfungo wa ramadhani waliomba sherehe hizo zisogezwe mbele, na sasa ombi lao limekubaliwa na sherehe hizo zitafana.

'Nina imani wanayanga wote watajumuika katika sherehe hizo za kutimiza miaka 80 ya kuzaliwa Yanga na vile vile kufurahia ubingwa wetu wa 25 wa ligi kuu bara', alisema Tiboroha.

ILIPOTOKEA YANGA HADI LEO HII

Ingawa historia inasema Yanga ilianzishwa mwaka 1935 na Simba mwaka 1936, lakini ukizama ndani utagundua kwamba , huo ndiyo ulikuwa mwanzo wa utani na upinzani wa jadi baina ya miamba hiyo ya soka nchini.

Kulikuwa kuna timu inaitwa New Youngs ambayo mwaka 1938 ilisambaratika na baadhi ya wachezaji wake wakaenda kuunda timu iliyokuwa Sunderland, ambayo hivi sasa inajulikana kama Simba.

Kabla ya kutokea vurugu zilizoisambaratisha New Youngs vijana wa Dar es Salaam walikuwa na desturi ya kukutana viwanja wa jangwani kufanya mazoezi na baada ya muda wakaamua kuunda timu yao, waliyoipachika jina Jangwani Boys.

Ndani ya kipindi kifupi timu hiyo iliteka hisia za wengi, waliojitokeza kujiandikisha uanachama wa klabu hiyo, miongoni mwao waliovutiwa na uanachama wa klabu hiyo ni Tabu Mangala (Sasa marehemu) na ilipofika mwaka 1926 walifanya mkutano wa kwanza katika eneo ambalo hivi sasa kuna shule ya sekondari ya Tambaza.

Miongoni mwa yaliyojadiliwa kwenye mkutano huo ni kuiboresha timu hiyo ambayo wachezaji wake wengi walikuwa wafanyakazi wa bandarini na mashabiki wake wengi walikuwa wabeba mizigo bandarini.

Baada ya mkutano huo, timu ilibadilishwa jina na kuwa Navigation, iliyotokea kuwa moto wa kuotea mbali katika timu za waafrika enzi hizo, kabla ya uhuru wa Tanganyika.

Timu kama Kisutu, Kitumbini, Gerezani na Mtendeni zilikuwa hazifui dafu kwa wana wa Jangwani hao.

Enzi hizo kikosi cha Yanga cha ushindani kikiwa uwanjani tayari kwa mchezo

Ikiwa inatamba kwa jina la Navigation, wanachama wa timu hiyo walikuwa wanatembea kifua mbele na kuwatambia wapinzani wao, kwamba katika kipindi hicho wao ndiyo zaidi, kwa sababu Italia ilikuwa inatamba kwenye ulimwengu wa soka, wanachama wa timu hiyo nao waliamua kuibadilisha jina timu yao na kuiita Italiana.

Taliana FC ilipata mafanikio ya halaka na haikushangaza ilipopanda ligi Daraja la pili kanda ya Dar es Salaam.

Mwanzoni mwa miaka ya 1930 Taliana waliamua kuachana nalo mapema kabla ya kuingia kwenye ligi hiyo, hivyo wakaanza kujiita New Youngs.

Kila kila ilipokuwa ikibadilisha jina, ilikuwa ikifanya vitu vipya pia, kwani wakiwa na jina la New Youngs waliweza kutwaa kombe la Kassum, lililoshirikisha timu mbalimbali za Dar es Salaam.

Hatimaye ukawadia mwaka mbaya kwa New Youngs 1938 wakati baadhi ya wachezaji walipojitoa na kwenda kuanzisha Sunderland.

Kwa sababu hiyo, waliobaki wakaamua kubadili jina na kuwa Young Africans jina ambalo mashabiki wake wengi walishindwa kulitamka vizuri hivyo kujikuta wakisema Yanga.

Miaka ya 80 baadaye leo, ni timu ya kihistoria Tanzania ikiwa inaongoza kutwaa ubingwa wa ligi kuu Tanzania bara kwa mara 25.

Pongezi nyingi ziwaendee wachezaji wote waliopata kuichezea timu hiyo kuanzia enzi za Jangwani Boys, Navigation, Italiana, New Youngs hadi leo hii ikijulikana kama Yanga ingawa katika cheti chake cha usajili inafahamika kama Dar Young Africans.

Mafanikio ya Yanga ndani ya miaka 80 hayakuja hivi hivi bila kuwapongeza viongozi ambao waliihangaikia timu hiyo inasimama kidete, viongozi wa enzi hizo hadi leo hii wanastahili pongezi kwa kuiwezesha kutwaa mara nyingi ubingwa wa nchi.

Wachezaji wa zamani wa Yanga ambao kwa sasa wameunda timu yao ya Yanga veterani

Shukrani nyingine ziwaendee wanachama, wapenzi na mashabiki, bila kuwasahau waandishi wa habari, bila hamasa zao sidhani kama Yanga ingeweza kufika hapo ilipo, hiyo ndiiyo historia ya klabu ya Yanga ambayo ndio iliyozaa Sunderland leo hii ikiitwa Simba SC.

Nania angeijua Simba kama si Yanga, hivyo inajivunia ubora ilionao, Yanga imetoa viongozi mbalimbali wa soka na serikali mmoja wapo ni rais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Jakaya Mrisho Kikwete ambaye mwaka 1976 alipokuwa mwenyekiti wa kamati ya usajili wa klabu hiyo na kuwezesha usajili wa Shaaban Katwila.

Pia Yanga imetoa rais wa CECAFA Leodegar Tenga, rais wa TFF Jamal Malinzi, nahodha wa Taifa Stars na Zanzibar Heroes Hadir Haroub 'Cannavaro'na kocha wa timu ya taifa, Taifa Stars Charles Boniface Mkwasa na wengineo.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC