Ruka hadi kwenye maudhui makuu

THE GUNNERS WATUPWA NJE ULAYA

Pamoja na kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 wakiwa ugenini katika mchezo uliopigwa usiku wa kuamkia leo, washika bunduki wa jiji la London Arsenal wameshindwa kusonga mbele katika hatua ya robo fainali ya mashindano ya klabu bingwa barani Ulaya kwa kosa la kuruhusu magoli mengi wakiwa nyumbani katika mchezo wa awali, ambapo Monaco iliwabamiza wenyeji wao hao Arsenal kwa jumla ya mabao 3-1.

Arsenal ilijipatia goli la kwanza dakika ya 36 ya mchezo huo kupitia mchezaji wake Olivier Giroud kabla ya Aaron Ramsey kuongeza la pili katika dakika ya 79 ya mchezo huo. Matokeo ya jumla kwa timu hizo ni 3-3 japo Monaco inasonga mbele kwa faida ya kuwa na magoli mengi ya ugenini na kuwaacha vijana wa mzee Wenga wakikosa kufika robo fainali kwa mara ya tano mfululizo.


Kitimtimu hicho cha klabu bingwa Ulaya kilitimua vumbi pia huko nchini Hispania pale, Atletico Madrid ilipowakaribisha Bayer Leverkusen kutoka Ujerumani.

Katika mchezo huo wenyeji Atletico wamefanikiwa kusonga mbele kwa mikwaju ya Penati baada kumaliza dakika 120 wakiwa mbele kwa bao moja ambalo halikutosha kuamua mshindi kutokana na matokeo ya mchezo wa awali ambapo Leverkusen iliibanjua Atletico bao moja kwa bila.

Wakiwa mbele ya mashabiki wao lukuki Atletico ilishinda penati 3 dhidi ya 2 za wageni wao na kutinga moja kwa moja katika hatua ya robo fainali wakiungana na ndugu zao Real Madri.

Ligi hiyo itaendelea tena leo hii kwa michezo miwili kupigwa. Borussia Dortmund watavaana na Juventus huku miamba ya soka ya Hispania Barcelona ikiialika Manchester City kutoka England.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

Ngao ya Jamii sasa ni Simba na Yanga

Shirikisho la mpira wa miguu Tanzania TFF limebadilisha kanuni za mashindano za Ngao ya Jamii kutoka timu nne na sasa utaratibu utakuwa kama zamani. Bingwa wa Ligi Kuu bara atacheza na mshindi wa kombe la CRDB Cup "CRDB Federation Cup, na endapo kama bingwa wa ligi na CRDB atakuwa ni mmoja basi mshindi wa pili kwenye Ligi Kuu ya NBC atacheza mchezo wa ufunguzi wa ligi yaani Ngao ya Jamii.  Hivyo ni rasmi ufunguzi wa wa ligi kuu mchezo  wa "Ngao ya Jamii msimu huu 2025-2026 ni Yanga na Simba watakutana.

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...