Ruka hadi kwenye maudhui makuu

MAKALA: G-BOY ALIA NA MAPRODYUZA, ADAI WANAWAPUUZA WASANII CHIPUKIZI

Na Robert Michael
0752 711688

ANAITWA Julius George Mgomela (Pichani) ila maskani kwake Tabata Kisukuru humfahamu kwa jina la G-boy ambalo analitumia kwenye shughuri zake za muziki.

Tayari G-boy amerekodi nyimbo mbili ambapo moja inaitwa 'Pesa mke wangu'na nyingine inaitwa Promise, nyimbo zote hizo amemshirikisha PNC na amefanyia katika studio za Iringa Record chini ya prodyuza Tudi Thomas.

G-boy ambaye ni mwenyeji wa mkoa wa Kigoma amelalamikia ukata wa fedha ambapo amedai anaomba mdhamini ajitokeze ili aweze kuendeleza kipaji chake.

'Tatizo linalinisumbua ni ukata, sina pesa hivyo inanifanya nishindwe kupanga kazi zangu vizuri', alisema, Aidha G-boy anaelezea ukata wa fedha unamnyima fulsa ya kushirikiana na wasanii wakubwa kama vile Diamond Platinum.


G-boy amesema muziki unalipa hivyo endapo atapata menejiment atafanya mambo makubwa, G-boy anafanya muziki wa hiphop na Rnb na amepitia changamoto mbalimbali.

Akitoa maoni yake kwa upande wa serikali, G-boy amesema kuwa serikali imeshindwa kutoa hakimiliki kwa wasanii chipukizi na kupelekea kuibwa kwa kazi zao kiloa kukicha na wasanii wakubwa.

Aidha pia amelaani vitendo wanavyofanyiwa na baadhi ya maprodyuza ambao wamekuwa na tabia ya kuwacheleweshea kazi zao kwa vile ni 'Underground' na kuwathamini wasanii wakubwa.

'Mimi imeshenitokea wakati naenda studio kutengeneza wimbo wangu mmoja (Siyo huu wa sasa) nilipofika studio hiyo nikaambiwa nilipie gharama zao nikafanya hivyo, lakini sikufanikiwa kurekodi zaidi nikapigwa kalenda miezi nane', alisema na kuongeza.

'Baada ya kupigwa kalenda ikanilazimu nitumie unabe wangu wa kitaani (anacheka) ambapo nilimfosi prodyuza anitengenezee ngoma yangu au anirudishie fedha zangu', aliendelea G-boy.

'Kilio changu kwa maprodyuza waache dharau kwani na sisi tunahitaji kufika kwenye mafanikio kama waliyokuwa nayo hao wasanii maarufu, naamini nikitendewa haki nitafanya vizuri kwani uwezo ninao tena mkubwa', alimaliza.

Kwa sasa G-boy anajifua vikali kujiandaa na shoo mbalimbali zilizo mbele yake huku akiendelea kulilia wadhamini ili waweze kumsaidia mambo muhimu ikiwemo kumlipia gharama za studio na mavazi.

Machapisho maarufu kutoka blogu hii

HISTORIA YA TIMU YA MASHUJAA YA KIGOMA, KUMBE NI SHEA YA JESHI NA WANANCHI

Timu inaitwa Mashujaa Lake Tanganyika FC ( Mashujaa FC ) ilianza rasmi kampeni yake ya kupanda Ligi Kuu tarehe 29/9/2018 na imepanda Ligi Kuu 25/06/2023 miaka mitano ya kupambana kwenye Ligi Daraja la kwanza Championship. Timu hii inaendeshwa kwa ushirikiano wa pande mbili kati ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji kwa niaba ya Wananchi wa Kigoma. Muelewe hapa maana wengi wanasema ni timu ya Jeshi asilimia 100% Nembo ya timu ni Sokwe Dume, Shujaa wa Hifadhi za Gombe na Mahale zilizopo mkoani Kigoma. Rangi ya kwanza ya jezi ya timu (first kit) ni hiyo hapo chini na kwenye nembo ya timu ni rangi za tunda la michikichi (mawese ). Hii kama njano ni mawese yaliyoganda na huo wekundu ni mawese ya moto. Ukishika tunda la Mse juu utaona wekundu na ukikata katikati utaona njano. Nyeupe ni ‘nazi’ ya Mse hizi ni alama za utajiri wa Kigoma Jezi nyingine ni blue inayowakilisha Ziwa Tanganyika na Jezi nyingine ni Nyeupe

MAKALA: SIMBA NI TIMU YA KWANZA TANZANIA KUINGIA NUSU FAINALI AFRIKA

Na Prince Hoza AFISA Habari wa klabu ya Yanga SC Ally Shabani Kamwe alidiriki kuudanganya umma wa wapenzi wa soka hapa nchini kwamba hakuna timu yoyote hapa Tanzania kuwahi kuingia hatua ya nusu fainali ya vilabu Afrika. Kamwe alisema timu yake ya Yanga itakuwa timu ya kwanza nchini kuingia nusu fainali ya Afrika, Yanga ilikuwa inakaribia kabisa kutinga nusu fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika. Yanga ilianza vizuri ikiwa ugenini baada ya kuilaza mabao 2-0 timu ya Rivers United ya Nigeria, hivyo ilikuwa inasubiria mchezo wa marudiano uliofanyika uwanja wa kumbukumbu ya Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam. Kwa vyovyote Yanga walikuwa na uhakika wa kutinga nusu fainali kwani walihitaji sare yoyote ama ushindi wa aina yoyote. Hapo ndipo Afisa Habari wa Yanga, Ally Kamwe aliamua kupiga vijembe kwa watani zake Simba SC na kuipotosha jamii kwa kudai kwamba Yanga itakuwa timu ya kwanza Tanzania kuingia nusu fainali ya Afrika. Kamwe ameifuta hadi rekodi ya Simba kuwa timu ya kwanza Tan...

Mabululu ni wa Simba SC

Simba wameweka donge nono kunasa saini ya mshambuliaji Agostinho Cristovan Paciencio Mabululu anayekipiga Al Tripoli ya Libya Ili ajiunge na Wekundu hao wa Msimhazi. Simba wamefanya mazungumzo ya moja kwa moja na wakala wa Mabululu na mchezaji mwenyewe na wako tayari kulipa kiasi cha juu zaidi kunasa saini ya mshambuliaji huyo hatari zaidi Simba wanahitaji kumalizana na mshambuliaji huyo badala ya kumaliza fainali ya kombe la Shirikisho, tayari Crecentius Magori yuko nyuma ya mpango huo kuhakikisha Simba ijayo inatisha. Mbali na Mabululu, Simba pia inahitaji Saini ya kiungo mshambuliaji wa Azam FC Feisal Salum "Feitoto" ambaye pia amewahi kuichezea Yanga SC